Mfanyakazi mmoja
wa ofisi ya Kituo cha Uchunguzi wa
Magonjwa ya Mifugo,kanda ya kaskazini,kilichopo jijini Arusha, Kandidi Mlingi,ambae
alipata ajali ya gari mwaka 2015 na kukatwa mkono wake wa kushoto hadi leo
anasotea malipo ya fidia ya ajali hiyo.
Mlingi,
ambae Septemba 18 mwaka 2015,majira ya saa 11.30 jioni ,wakati wa ajali alikuwa
akitokea eneo la Lokii wilayani Arumeru kukagua minada ya mifugo akiwa na
watumishi wenzake walikuwa wakisafiria kutumia gari aina ya Toyota Land
Cruiser, namba STJ 5929.
Gari hiyo
ilikuwa ikiendeshwa na Samweli Kambaine,iliacha njia na kupinduka kwenye bara
bara itokayo Lokii wilayani Arumeru ikirejea kwenye kituo cha utafiti wa
magonjwa ya mifugo kanda ya kaskazini mjini Arusha .
Miongoni mwa
wafanyakazi wengine waliopata ajali kwenye msafara huo ni pamoja na Nemes Msaki,ambapo yeye alipata majeraha kwa asilimia 17 huku Kandidi
alipata majeraha kwa asilimia 54 na dereva alipoteza fahamu.
Kulingana na
uchunguzi uliofanywa na daktari wa Hospital ya mkoa ya Mount Meru, Dkt Iddi
Mtengwa ,umebaini kiwango hicho cha majeraha waliyopata wafanyakazi hao sanjari
na aliyekuwa dereva kupoteza fahamu.
Ripoti ya
askari wa kikosi cha usalama barabarani cha wilaya ya Arumeru, kilichopo mji mdogo
wa Usa river,walithibitisha kuwa ajali hiyo ilikuwa ni mbaya na gari hilo
halifai tena .
Taarifa toka
ndani ya familia zimeeleza kusikitishwa kwao na wizara ya Kilimo, Mifugo na
Uvuvi,kutokuwa na mawasiliano na mtumishi huyo ambae kwa sasa hana mkono mmoja
.
Mke wa majeruhi Kandidi amesema tangu kutokea
ajali hiyo Septemba 2015 hakuna jitihada zozote zinazofanywa na Wizara
husika juu ya namna ya kumwekea mkono
bandia mume wake wala mawasiliano .
ARUSHA
WALIOKUWA wafanyakazi wa
kiwanda cha nguo cha Kilitex cha jijini Arusha,wamemuomba rais John Magufuli,
awasaidie waweze kulipwa stahiki zao ambazo hawakulipwa hadi leo tangia kiwanda
hicho kisitishe uzalishaji na kufungwa rasmi mwaka 2007.
Wakizungumza na
wanahabari, jijini Arusha,Mwenyekiti wa wa Wafanyakazi hao Shabaan Tandala, na
katibu wake Nathaniel Longida, wamesema wameshapeleka kilio chao hicho kwa
mamlaka mbalimbali za serikali lakini hadi leo hawajapata ufumbuzi .
Wamesema katika harakati
zao hizo walijibiwa na Ikulu kwa barua kumb namb STJ/MIL/1 ya
29/2/2007ambapo Ikulu iliandikia Wizara ya Fedha kwa barua namb
CEA/404/10/01 ya 8/10/2007iliyosainiwa na aliyekuwa katibu wa rais, Masaju,kwenda
wizara ya fedha ili waweze kulipwa lakini hadi leo .
Wamesema Novemba 26/2007
walipokea barua nyingine toka Ikulu namb C/CA 251/473/01 iliyosainiwa na
Mahushi kwa niaba ya Katibu mkuu Hazina ikisisitiza kulipwa stahiki
zao ,ambazo hawajalipwa hivyo
wamelazimika kupeleka kilio chao kwa rais Magufuli,ili awasaidie wapate stahiki
hizo.
Kwenye barua yao ya
wamemuomba rais kuwasaidia kupata stahiki hizo kwa kuwa kuna dalili za kutopata
stahiki zao.
Wamesema mwezi May mwaka
2015 ,walimkabidhi barua yao Katibu mkuu wa CCM, Abdulhaman Kinana ,wakimuomba
awasaidie kuifikisha kilio chao kwa rais Jakaya Kikwete, ili waweze kulipwa
lakini hadi leo kimya.
Wamesema kutokana na
ukimya huo ambao unawajengea hofu na mashaka kutokana na kutolipwa wanamuomba
rais Magufuli, awasaidie waweze kupata stahiki zao.
Wamesema wakati kiwanda
kinabinafisishwa kupitia PCRC, walikuwa waanyakazi zaidi ya 200 lakini sasa
wamebakia wachache kwa kuwa wengine wamefariki dunia bila ya kulipwa stahiki
zao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni