Mahakama
ya hakimu mkazi Arusha, imeiagiza serikali kukamilisha upelelezi wa
kesi ya uchochezi inayomkabili mbunge wa jimbo la Arusha, Godbless Lema,
Chadema, ndani ya siku 60 ambapo imepangwa Novemba 15 mwaka huu
vinginevyo itatoa maamuzi mengine.
Hakim
mkazi mfawidhi, Augostino Rwezile, ametoa agizo hilo leo katika
mahakama hiyo ambayo ilikuwa imekaa tayari kwa kuanza kusikiliza kesi
hiyo kabla ya wakili wa serikali kuomba iahirishwe kutokana na upelelezi
kutokukamilika.
Awali
wakili wa serikali Blandina Msawa, aliiambia mahakama hiyo kuwa
upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba kupewa siku 60 ili
kukamilisha upelelezi huo.
Wakili
wa mlalamikajhi, John Malya, ameiambia mahakama kuwa anashangaa kuona
upelelezi unachukua muda mrefu wakati simu ya mbunge huyo imeshikiliwa
na polisi kwa kipindi kirefu.
Ameiambia
mahakama kuwa simu hiyo ndio iliyotumika kusambaza maneno ya uchochezi
kama inavyodaiwa na serikali, hivyo yeye anashangaa kuona kesi ikichukua
muda mrefu
Kwa
upande wake Lema, ameiomba mahakama kumpatia muda wa kutosha ili aweze
kuhudhuria vikao vya bunge la Jamhuri mwezi ujao mjini Dodoma, ili aweze
kupata muda pia wa kuhudhuria kesi yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni