Wakazi wa Kijiji cha Kisesa Kata ya Vudee wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa shambala Mirungi
Mkulima
wa zao la Mirungi Johnson Charles Kangara akiwa ameshika mafuta ya taa
tayari kwa ajili ya kuteketeza shamba lake la Mirungi
Shamba la Mirungi likiteketea baada ya agizo la Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki
Dc Staki akiwasisitiza wananchi kutojihusisha na kilimo cha zao la Mirungi
Na Mathias Canal, Kilimanjaro
Mwishoni
mwa mwezi Septemba mwaka huu Uongozi wa Wilaya ya Same ulitangaza vita
dhidi ya wakulima wa Bangi, na Mirungi huku akitangaza kuwa kifungo cha
miaka 30 kitawahusu wakulima wote wanaojishughulisha na kilimo hicho
haramu kwani Bangi na Mirungi ni hatari kwa afya za watumiaji na
kuisababishia serikali hasara kwa kutopokea Kodi.
Kiama
hicho kilitangazwa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki
Senyamule wakati akikabidhiwa mradi wa Ruvu muungano uliojumuisha
zahanati sita, Nyumba mbili za waganga, matanki saba ya kuvuna maji na
madarasa 54, ofisi 16 za walimu, vyumba na vyoo vya chuo cha ufundi
makanya uliofadhiliwa na shirika la World Vision Tanzania.
Dc
Staki alisema kuwa kwa asilimia kubwa serikali imekuwa ikiwadhibu
wanaoingiza Mirungi na Bangi sokoni huku ikiwasahau kuwachukulia hatua
wale wote wanalima zao hilo.
Hivi
karibu katika kijiji cha kisesa kata ya Vudee Wilayani humo ilibainika
kuwa kuna wakulima wa Mirungi ambao wanajihusisha na zao hilo kwa muda
mrefu pasina serikali kuwabaini na kuwa sugu kwa kilimo hicho hatimaye
kukiona kama kilimo cha halali.
Dc Staki alipotangaza kiama cha kukabiliana na wale wote wanaojihusisha na kilimo hicho aliahidi kuwatafuta wakulima hao na hatimaye kuwachukulia hatua za kisheria na kuhakikisha kuwa Wilaya ya same inakuwa safi pasina kuwa na Mirungi.
Hata hivyo katika ziara yake ya kazi Mhe Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki alipozuru kijiji cha kisesa kata ya Vudee alifanikiwa kumuweka chini ya ulinzi mkulima wa zao la Mirungi Johnson Charles Kangara na hatimaye kumuelekeza kuwasha kiberiti yeye mwenyewe katika shamba zima na kuchoma zao hilo.
Dc Staki ameahidi kuhakikisha Wilaya ya Same inasifika kwa kilimo cha mazao mengine rafiki katika jamii ya Biashara na chakula na kuteketeza mazao yote haramu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni