Watu
10 wamefariki dunia na wengine 44 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni
ya Barcelona walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es Salaam kwenda
mkoani Lindi kupata ajali eneo na Miteja mkoani Lindi.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renata Mzinga imesema kuwa chanzo cha ajali hiyo kimetokana na tairi ya gari ya upande wa kushoto kupasuka na kutokana na mwendo wa kasi wa basi hilo, dereva alipoteza uelekeo ndipo likapinduka.
Pia
Kamanda Mzinga amesema kuwa wamechunguza na kugundua kua licha ya kuwa
basi hilo lilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 48, wakati basi hilo
linapata ajali kulikuwa na abiria 54 kitu ambacho ni kosa kisheria.
Aidha,
Kamanda Mzinga amesema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi kuweza
kubaini alipo dereva ili kuweza kufahamu ni kipi hasa kilichotokea. Hadi
sasa wanamshikilia kondakta wa basi hilo lakini bado hajaweza kuelezea
tukio halisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni