Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza kushoto) akimshkuru
Meneja wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint
Venture Ltd, baada ya kuhakiki msaada wa mabati 500 na mifuko ya saruji
500.
Na Mahmoud Ahmad - Arusha
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepokea
msaada wa bati 500 pamoja na mifuko ya saruji 500 kwa ajili ya kuwezesha huduma
mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati pamoja na shule za msingi na
sekondari za Mkoa wa Arusha.
Mara baada ya kukabidhi wa msaada huo nje ya jengo la Ofisi ya Mkuu huyo, Gambo
alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Dararro mifuko 100 ya saruji
na mabati 100 kwa ajili ya ujenzi kituo cha afya kinachojengwa eneo la
kwa mama mbauda kata ya Muriet Jijini Arusha.
Alisema msaada huo utawezesha kila wilaya kunufaika nao kwani kila wilaya za
mkoa wa Arusha kuna changamoto za uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na
mahitaji ya majengo ya zahanati ili kusogeza huduma kwa wananchi.
Alimshukuru Meneja Mradi wa Kampuni ya ujenzi ya Hanil - Jiangsu Joint Venture
Ltd, inayojenga barabara ya Sakina -
Tengeru Km 14.1 na barabara ya Mchepuko Km 42.4 , Xie Jianbao ambao wametoa
msaada huo kama sehemu ya kurudhisha kwa jamii ya watanzania ili kukuza
mahusiano na kujali jamii na Taifa ambalo limewapa kazi kubwa ya ujenzi wa
barabar hiyo itakayogharimu takribani Bil. 139.
"Naishukuru kampuni hii kwa kutoa msaada huo kwa ajili ya kuleta maendeleo
na naahidi tutautumia ipasavyo katika kuleta maendeleo na kila wilaya
nitakayofanya ziara msaada huo nitaupeleka ili ya kupunguza changamoto
mbalimbali kwa jamii ".
Naye Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Bw. Xie alisema kampuni yao imeona umuhimu
wa kuchangia jamii kwani wao ni wajenzi wa barabara na wanastahili kurejesha
faida kwa jamii inayowazunguka.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro alimshukuru Gambo kwa
msaada huo na kusisitiza kuwa mifuko hiyo 100 ya saruji pamoja na bati
100 zitasaidia ujenzi wa kituo cha afya kinachojengwa Kata ya Muriet
Jijini Arusha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia alishukuru kwa msaada huo
utakaosaidia ujenzi wa kituo cha afya kujengwa na kukamilika ndani ya miezi
miwili na kuahidi kwamba atasimamia ipasavyo ili kuhakikisha Kituo kinajengwa
katia ubora unaostahili.
Katika
makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na wabunge wa Viti maalum wanawake Mkoa wa
Arusha, Catherine Magige na Aminah Mollel walitoa rai kwa nyakati tofauti kwa
wananchi wa mkoa wa Arusha kumuunga mkono Mhe. Gambo pamoja na Serikali ili
kuwezesha maendeleo kusonga mbele.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni