Mshambuliaji wa Ubelgiji, Christian Benteke, amefunga goli la mapema mno kuwahi kufunga katika hatua ya kuwania kufuzu kuntinga michuono ya kombe la dunia baada ya kufunga katika sekunde ya saba dhidi ya Gibraltar.
Mshambuliaji huyo wa timu ya Crystal Palace pia katika mchezo huo amefanikiwa kutikisa nyavu mara tatu yaani hat-trick wakati Ubelgiji ikishinda kwa ushindi mnono wa magoli 6-0 katika mchezo wa kundi H.
Kwa goli hilo la Benteke limeipita rekodi ya goli lililoweka rekodi ya kufungwa mapema katika michuano hiyo lililofungwa sekunde ya 8.3 na Davide Gualtieri wa San Marino dhidi ya Uingereza mwaka 1993.
Axel Wisel akishangilia goli la pili alilofunga kwa shuti la mita 25
Katika mchezo mwingine wa kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 kiungo wa Manchester United, Paul Pogba ameifungia Ufaransa goli la shuti la mbali na kuisaidia kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Uholanzi.
Mpira uliopigwa na Paul Pogba ukitinga wavuni huku kipa wa Uholanzi akiwa ameanguka chini asijue la kufanya
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni