![]()  | 
| DC-Longido,Mh Chongolo. | 
Mkuu
 wa wilaya ya Longido Daniel Godfrey Chongolo amemtia ndani Mkandarasi 
anayejenga barabara ya Longido-Kitumbeine-Oldonyolengai Bw. Loserian 
Sokonei Mollel kutokana na uzembe na kutotimiza matakwa ya mkataba na 
kuwasababishia usumbufu watumiaji wa barabara hiyo pamoja  na wananchi 
kwa ujumla. 
Mkandarasi
 huyo anayemiliki kampuni ya Genuine Company Limited amekuwa akiendesha 
shughuli za ujenzi wa drift katika barabara hiyo bila kutengeneza 
barabara mchepuko (diversion) katika maeneo hayo na kusababisha mara kwa
 mara wasafiri kukwama na kulala porini. 
Wakizungumza
 na mtandao huu, wananchi wa kijiji cha Gelai Lumbwa wamepongeza uamuzi 
wa DC Chongolo kwa sababu unasaidia kuondosha na kutatua kero 
zanazowasumbua na kuwakwaza kwenye maisha yao ya kila siku. "Tulichoshwa
 na watu waliokuwa wakifanya mambo vile wanavyotaka wao. Kwa hakika hii 
ni awamu ya Kazi Tu, tunamshukuru DC na OCD na tunamuunga mkono" alisema
 Mesiaki Laizer.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni