HUDUMA
za upimaji afya bure zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Vijana yanayokwenda sambamba na tukio la
uzimaji Mwenge zimekuwa kivutio kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu.
Mfuko
unatoa huduma za vipimo vya shinikizo la damu, kiwango cha sukari,
uzito na urefu lakini pia mwananchi anayepima anapata fursa ya kupata
elimu ya namna ya kujikinga na maradhi yasiyoambukiza kwa kuzingatia
mtindo bora wa maisha.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti bandani hapo, wananchi hao wamesema, kitendo
kilichofanywa na Mfuko cha kusogeza huduma hiyo mkoani humo ni nzuri kwa
kuwa inawapa fursa ya kujua hali ya afya yao.
“Kwa
kweli niwapongeze sana kwa huduma hii ambayo mnatupima bila ya kutoa
gharama yoyote lakini kitu kizuri Zaidi ni kupata elimu ya namna ya
kuishi ili kuepukana na maradhi ambayo yanaweza kuepukika kwa kuzingatia
ushauri wa wataalam ambao leo tunaupata bila gharama yoyote,” alisema
Bw. Maduhu Sita mkazi wa Bariadi.
Akizungumzia
mwitikio wa wananchi bandani hapo ambao wanafika kwa lengo la kupata
huduma ya vipimo, Meneja wa NHIF Mkoa wa Shinyanga na Simiyu Bw. Imanuel
Amani alisema kuwa mwitikio wa wananchi ni mkubwa sana.
“Mwitikio
kwa kweli ni mkubwa sana nah ii inaonesha tu kwamba wananchi wanataka
kujua hali ya afya zao na kwa upande wetu NHIF tupo tayari kuwahudumia
hawa wananchi kwa kadri itakavyowezekana hivyo hata ambao hawajafika
hapa waje ili tuwahudumie,” alisema.
Alieleza
kuwa mbali na upimaji wa afya, Mfuko pia unatumia nafasi hiyo
kuwahamasisha wananchi kujiunga na huduma zake ili wawe na uhakika wa
kupata matibabu wakati wowote.
“Kwa
sasa NHIF imepanua wigo wake ambapo makundi mbalimbali yanaruhusiwa
kujiunga na huduma zake yakiwemo makundi ya wajasiliamali, watoto,
wanafunzi, watu binafsi hivyo nawaomba wananchi wafike bandani kwetu ili
tuwahudumie,” alisema Bw. Amani.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka akipima kipimo cha shinikizo la damu
wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwenye
maonesho ya Wiki ya Vijana yanayoendelea mkoani humo.
Meneja
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Imanuel Amani akitoa elimu kwa
wananchi waliofika bandani hapo kujua huduma zinazotolewa na Mfuko.
Maofisa wa NHIF wakiendelea na kuwahudumia wananchi waliofika bandani hapo.
Wananchi wakiendelea na upimaji wa huduma za afya ndani ya banda la NHIF
Wananchi wakisubiri kupata huduma ya kupima afya zao
Huduma za upimaji zikiendelea
Wananchi mkoani Simiyu wakiwa na hamu ya kupata huduma za upimaji,
Wananchi wakijisajili kwa ajili ya kupata huduma ya upimaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni