Waziri
wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, ajira na wenye ulemavu
Jenista Mhagama, akizungumza na Vijana na Wananchi wa Mkoa wa Simiyu
wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa mwaka 2016, Mjini Bariadi.
Baadhi
ya Vijana wa Mkoa wa Simiyu wakionesha mabango yenye jumbe mbalimbali
kwa Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, ajira na
wenye ulemavu Jenista Mhagama ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi
wa Wiki ya Vijana Mjini Bariadi.
Kikundi
cha Brass Band cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani Dar es Salaam
wakiwaongoza vijana katika maandamano ya amani kuelekea uwanja wa
Sabasaba Mjini Bariadi ambapo wiki ya vijana imezinduliwa rasmi leo.
Waziri
wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, ajira na wenye ulemavu
Jenista Mhagama (wa tano kushoto) viongozi mbalimbali ngazi ya taifa na
Mkoa wakipokea maandamano ya vijana katika Uzinduzi wa Wiki ya Vijana,
Uwanja wa Sabasaba Mjni Bariadi.
Baadhi
ya Vijana wa Mkoa wa Simiyu wakiwa wamebeba bango wakielekea uwanja wa
Sabasaba,Mjini Bariadi mahali ulipofanyika Uzinduzi wa Wiki ya Vijana
kitifa mwaka 2016.
Waziri
wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, ajira na wenye ulemavu
Jenista Mhagama, akivishwa skafu na vijana wa skauti wa Mkoa wa Simiyu
kabla ya kupokea maandamano ya amani ya vijana katika Uzinduzi wa Wiki
ya Vijana, Uwanja wa Sabasaba Mjni Bariadi.
Picha
four:Kikundi cha Brass Band cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani
Dar es Salaam wakiwaongoza vijana katika maandamano ya amani kuelekea
uwanja wa Sabasaba Mjini Bariadi ambapo wiki ya vijana imezinduliwa
rasmi leo.
Vijana
wa Halaiki wakiwa katika katika maandamano ya amani kuelekea uwanja wa
Sabasaba Mjini Bariadi ambapo wiki ya vijana imezinduliwa rasmi leo.
Na Stella Kalinga Simiyu.
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, ajira na wenye ulemavu
Jenista Mhagama ameziagiza halmashauri zote nchini ambazo hazijatenga
maeneo kwa ajili ya vijana kufanya hivyo mara moja.
Mbali
na hilo Mhagama ameziagiza halmashauri nchi nzima kuhakikisha
zinafungua na kuanzisha SACCOS za Vijana na kuzisimamia ili vijana
wapate mikopo yenye masharti nafuu, ikiwa pamoja na kuhakikisha
zinatenga asilimia 5 ya mapato ya ndani kama inavyotakiwa.
Waziri
Mhagama alitoa maagizo hayo Mkoani Simiyu wakati akiongea na mamia ya
wananchi na vijana wa Mkoa huo mjini Bariadi katika ufunguzi wa
maadhimisho ya wiki ya vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani hapa.
Mhagama
amesema kuwa mpaka sasa ni halmashauri 72 zimeshatenga hekari 84037
kati 185 kwa ajili ya vijana katika shughuli za kilimo, ufugaji na
kibiashara, ili kuweza kujiletea maendeleo ya kiuchumi.
“
..kupitia maadhimisho haya ninaagiza halmashauri zote nchini ambazo
zinafahamu bado hazijatenga maeneo haya kuhakikisha wanatenga mara
moja…na kuwapatia vijana kwa ajili ya kufanya shughuli hizo” Alisema
Waziri
Aidha
Waziri huyo aliongeza kuwa bado kuna halmashauri nchini zimeshindwa
kutekeleza maagizo ya serikali ya kuanzisha SACCOS za Vijana, ambapo
mpaka sasa ni halmashauri 113 tu ambazo zimeanzisha SACCOS hizo kati ya
185, huku zikiwa zimetenga jumla ya shilingi Bilioni.3.9 kwa mwaka wa
fedha 2016/17 na akazitaka halmashauri zingine kuanzisha SACCOS hizo na
kutenga fedha za Vijana mara moja.
Awali
akimkaribisha Waziri huyo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka
amesema kuwa mkoa huo umeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli la
kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda kwa kuanzisha viwanda viwili vidogo;
kiwanda cha kutengeneza chaki kilichopo wilaya ya Maswa na cha
kusindika Maziwa kilichopo Meatu.
Mtaka
amesema Serikali mkoani humo imedhamiria kuufanya mkoa huo kuwa wa
mfano na kuwa miongoni mwa mikoa mitano ya kutumainiwa kibiashara ambao
viongozi mbalimbali wataenda kujifunza namna unavyotekeleza.
Hata
hivyo Waziri Mhagama alimpongeza Mkuu wa mkoa huyo na kusema kuwa
amekuwa kiongozi wa kwanza kutekeleza agizo la Rais, na kumuahidi kuwa
ofisi ya Waziri Mkuu iko tayari kusaidia juhudi hizo hata kwa kutoa
fedha za kuwawezesha vijana.
Kwa
upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia wenye
ulemavu amewataka Wakuu wa mikoa , wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa
Halmashauri kote nchini kuwa chachu na kiungo muhimu katika kuandaa
na kutekeleza mikakati ya kutokomeza unyanyapaa na vitendo vya ukatili,
wanavyofanyiwa watu wenye ualbino ili nao waweze kufanya shughuli za
maendeleo bila uoga kama ilivyo kwa baadhi yao.
Wiki
ya vijana itahitimishwa pamoja na Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu
ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, tarehe 14
Oktoba, 2016 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni