Kiongozi
mkuu wa kanisa la Ukombozi ,Nabii B.G Malisa akizungumza na waandishi
wa habari mara baada tu ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Kilimanjaro(KIA) leo ambapo atakuwa na mkutano wa maombezi wa siku 8
katika viwanja vya reli jijini Arusha
Umati wa wakazi wa
mkoa
wa Arusha waliofurika katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa
Kilimanjaro(KIA) kumpokea Nabii B.G Malisa ambaye atakuwa na mkutano wa
maombezi wa siku 8 katika viwanja vya reli jijini A
rusha
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Watanzania
wametakiwa kudumisha amani ya nchi kwa kuepuka kufanya matukio ambayo
yanaweza kuchochea vurugu na hatari ya kuliingiza taifa katika hali ya
machafuko.
Wito
huo umetolewa jana na mchungaji kiongozi wa kanisa la Ukombozi hapa
nchini, Nabii B. G Malisa wakati alipokuwa akihubiri neno la Mungu
katika viwanja vya reli jijini Arusha.
Nabii Malisa alisema kwamba watanzania wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanaombea amani ya nchi inaendelea kutawala hapa nchini.
Alisema
ya kwamba amekuwa akifanya ziara mbalimbali katika nchi mbalimbali
duniani na kushuhudia hali ya usalama ikiwa tete ambapo askari wamekuwa
wakitembea mitaani huku wameshika silaha za moto.
"Hivi
karibuni nilikuwa Nigeria wakati nashuka uwanja wa ndege nilipokelewa
na askari wenye silaha za moto nikajiuliza maswali mengi sana kuhusu
amani tuliyonayo hapa Tanzania "alisema Malisa
Hatahivyo,
alitoa wito kwa serikali kuunga mkono juhudi za viongozi mbalimbali wa
dini hapa nchini katika kuwasaidia vijana na kusema viongozi wa dini
wanafanya kazi kubwa katika kuwainua watu kiuchumi na kuwaepusha na
vitendo viovu.
Awali
akizungumza na waandishi wa habari mchungaji wa kanisa la Ukombozi tawi
la Arusha Mchungaji Ushindi alisema kwamba mhubiri huyo atakwenda
kufanya huduma ya maombezi mkoani Arusha kwa siku nane na kuwataka
wakazi hao kujitokeza kwa wingi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni