Bilionea wa Makasino, James Packer, ametengana na mchumba wake mwanamuziki nyota wa zamani nchini Marekani Mariah Carey.
Kwa mujibu wa jarida la Australian la Woman's Day, Packer, 48, amemtosa nyota huyo wa pop, 46, kutokana na kuwa na matumizi makubwa pamoja na kuwa na shoo yake ya maisha ya uhalisi ya Mariah inayoonekana duniani.
Kwa mujibu wa jarida hilo hata hivyo Packer, amemruhusu Mariah kuendelea kubakia na pete ya uchumba ya almasi yenye thamani ya dola milioni 10, sawa na karibu shilingi bilioni 22 za Tanzania.
Mariah Carey akiwa amevaa pete ya uchumba ya madini ya almasi yenye thamani ya dola milioni 10
Bilionea James Packer akiwa na mchumba wake Mariah Carey kabla ya penzi halijatumbukia nyongo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni