ASKARI WA TANAPA AWEKWA NDANI KWA KASHFA YA UBAKAJI

Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Halima Ally (28) mkazi wa kijiji cha
Moya mayoka amelalamikia kubakwa na askari wa wanyama pori Hifadhi ya ziwa
Manyara na kumtaka Rais Joseph Pombe Magufuli aingilie kati kutokana na
suala lake kufumbiwa macho na mamlaka husika.



Akizungumza   kwa uchungu kuhusiana na tukio hilo Halima amesema kuwa tangu
apate mkasa huo tarehe 5/10/2011 majiraya saa kumi na mbili jioni eneo la
kitongoji cha Mayoka “C” alipokwenda shambani kuokota kuni ndipo
alipokutana na dhahama hiyo.



Aidha  amesema  kuwa wakati akiendelea na zoezi la kuokota kuni katika Eneo
la shamba hilo linalomilikiwa na kijiji chenye usajili *No AR kij.29*ndipo
Bi Halima alipokamatwa na askari wa wanyama pori aliyefahamika kwa jina
moja Mwasomola akidaiwa kuingia katika Eneo la hifadhi.



Aliendelea kusema kuwa askari huyo kabla ya kumbaka alimtishia kwa bunduki
yake aliyokuwa amebeba hali iliyopelekea Bi Halima kuogopa na kukaa kimya
huku akihisi maumivu kutokana na hali ya ujauzito aliyokuwa nao kutokana na
askari huyo kuendelea kutekeleza azma yake hiyo ya ubakaji.



Ameongeza kuwa  baada  ya kitendo  hicho alikwenda   moja  kwa moja  kumweleza
mume wake aliyefahamika kwa jina la   Samweli   Bura  ambaye  aliambatana  na
mkewe  huyo  hadi kituo  cha   Poisi Magugu   ambapo  ilifunguliwa kesi   ya
kubaka yenye  jalada namba  MGG/RB/1673/2011 ambapo Polisi walikwenda
kumkamata  mtuhumiwa .



Mtuhumiwa baada ya kukamatwa   alpelekwa    kupimwa afya yake    na
kugundulika  kuwa hajaathirika na maambukizi  ya ukimwi , hivyo  katika  hatua
hiyo   Mkuu wa kituo   cha Polisi   Magugu  enzi hizo Thomasi Njuki   ambaye
kwa sasa  ni marehemu  , baada ya kuuwawa  kwa kupigwa risasi na
majambazi  wilayani Mkuranga  alipokuwa anaongoza  operesheni  ya kupambana
na    majambazi alimshawishi mlalamikaji amsamehe mshitakiwa kwa kuwa kesi
hiyo ingemfunga ambapo mlalamikaji alimsamehe mshitakiwa



‘’Vitendo  hivi vya unyanyasaji toka nilipopata mkasa wa kubakwa  vimekuwa
vikiendelea  hadi  sasa hivyo  tunaiomba serekali  kupitia Raisi  Magufuli
atusaidie  tuweze kupata haki  zetu’’ Alisema Bi  Halima .



Mwathirika mwingine aliyefahamika kwa jina la Ngasso Iddi (70) naye
alilalamikia unyanyasaji huo   kwa kukamatwa   na kupigwa na askari
wanyama  pori  huku  akilazimishwa   kuvua suruali  kisha kuchapwa  viboko
na kulazimishwa  kuchimba kaburi  kwa vidole bila kujua kosa lake   huku
akidaiwa   amechunga eneo la hifadhi ambapo mifugo  yake aina ya mbuzi
wapatao kumi na (11) walikamatwa na Askari  wa Hifadhi hiyo huku
akitozwa  faini
ya silingi elfu  sitini  iliyotjibitishwa  na receipt  No.  21079 ilitolewa
tarehe 21/06/2016.



Kufuatia mfululizo   wa matukio  hayo  ya unyanyasaji  baadhi ya wakazi
ambao  pia walipata  matatizo ya kubomolewa nyumba   zao   na
kunyang’anywa   maeneo yao   akiwemo  Samwel  Bura   ambaye alikuwa
miongoni mwa wakazi   wanaoishi katika  eneo  hilo  lenye kaya nane  mayoka
 ‘’C  alisema kuwa ameathirika kwakuwa amebomolewa  nyumba yake na
kulazmishwa kuondoka kwenye maeneo hayo ambayo yanadaiwa ni mali ya mamlaka
ya Hifadhi ya Taifa ambapo amepata hasara ya hekari sita za mahindi, ulezi
na mbaazi zenye jumla ya zaidi ya thamani ya  shilingi million kumi.



  Mbali ya athari hizo waathirika hao wamedai wameshambuliwa mara kwa mara
na wanyama pori licha ya mkazi  mmoja aliyefahamika kwa jina la Agustino
Masai  kuuwawa miaka ya nyuma na mbogo huku mazao ya wananchi aina ya
mahindi, maharage, ulezi na mbaazi yakiendelea kuharibiwa  vibaya na
wanyama kutoka katika hifadhi hiyo pasipo mamlaka ya hifadhi kulipa fidia
waathirika.



Waathirika hao ambao wamedai kuchoshwa na manyanyaso wanayofanyiwa na
mamlaka ya Hifadhi wameamua kupaza kilio  chao  kwa Rais Magufuli kupitia
vyombo vya habari ili waweze kupata haki yao kwa kuwa viongozi wa eneo hilo
wameshindwa kuwasaidia licha ya kuwasilishiwa malalamiko yao pindi
wanapopata athari katika mazao yao.



Mwenyekiti wa kijiji cha Moya Mayoka John Joseph ambaye pia ni Diwani wa
kata ya Magara Wilaya ya Babati amesikitishwa na ubabe wanaofanya TANAPA
kwakunyanyasa wakazi  waishio katika kijiji hicho chenye ekari  elfu tisa
mia nane na arobaini, na jumla ya wakazi  elfu mbili na mia nane, wakati
maeneo ya mashamba hayo yanamilikiwa kihalali na kijiji hicho.



Hata hivyo wakazi wa maeneo hayo wamekuwa na mashaka kwa risiti wanazopewa
baada ya mifugo yao kutozwa tozo kwa madai ya kuingia hifadhini wakidai
kwamba risiti hizo hazina namba ya mlipa kodi huku zingine zikiwa na muhuri
nyingine hazina huku akitoa mfano mwananchi Juma Swalehe aliyetozwa tozo ya
shilingi elfu hamsini na tano  tarehe 12/6/2016 na kupewa risiti namba
21079 risiti hiyo imegongwa muhuri lakini haina namba ya mlipa kodi na
risiti namba 21082 ya tarehe 21/6/2016 Mwananchi Ngao Iddi alilipa shilingi
elfu sitini na kupewa risiti hiyo ambayo haina namba ya mlipa kodi wala
muhuri.



Afisa wanyama pori Beatrice Ndanu alipohojiwa kuhusu taratibu za kulipa
fidia kwa waathirika wa wanyama pori wanaoharibiwa mifugo na mazao yao
alisema ikithibitika mtu ameuwawa na wanyama pori wategemezi wake
watapatiwa kifuta  machozi shilingi millioni moja, na aliyepata  ulemavu
atapewa Shilingi laki tano na athali nyingine ndogondogo ikithibitika
atapewa  shilingi elfu ishirini na tano  siyo fidia bali kifuta machozi.



Kamanda  wa Polisi wa mkoa wa  Manyara  Francis J. Massawe  alipohojiwa
kuhusiana na tukio  hilo alisema kuwa halijafika rasmi mezani kwake
ameahidi  kufuatilia zaidi  changamoto  hizo  ili kukomesha uhalifu  katika
maeneo  ya kijiji cha Moya  Mayoka ambapo ametoa wito  wananchi  kutokukaa
kimya, bali watoe  taarifa  hata  kwa siri  pindi wanapobaini vitendo  vya
uhalifu vinavyofanywa  dhidi  yao.

Afisa uhusiano wa shirika la Tanapa, Psscal Shelutete alipoulizwa kuhusu
vitendo vya unyanyasaji  vinavyotekelezwa na askari wa mamlaka ya hifadhi  kwa
kuwapiga watu  na kuwabaka pindi wanapokuwa wakichunga na kukata kuni  alisema
yeye siyo  msemaji wa masuala hayo bali sheria iko wazi  kwa  yeyote
anayevunja
sheria akilamikiwa sheria inapaswa kuchukua mkondo wake

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni