Habibu Mkalanga ,katika ofisi ya msajili viwatilifu (TPRI)na mratibu wa mafunzo mkoani Arusha. |
Na Mahmoud Ahmad Arusha.
Wito umetolewa kwa wadau
wote wa kilimo watumie viwatilifu vilivyosajiliwa na Taasisi ya
viwatilifu ya kufanya utafiti katika nchi za kitropiki (TPRI)kwani ubora
wake umehakikiwa na jinsi vinavyofanya kazi umehakikiwa pia.
Kauli hiyo imetolewa na
Habibu Mkalanga katika ofisi ya msajili wa viwatilifu na mratibu wa
mafunzo mkoani Arusha na kusema kuwa kabla ya kutumia viwatilifu ni
muhimu watumiaji waangalie matumizi kwenye vibandikao kama viwatilifu
hivyo ni vya wadudu au magugu,aina mavazi wanayotakiwa kuvaa kabla ya
kunyunyiza viwatilifu,kiasi kinachotakiwa, kisiwe chini ya kiwango wala
juu ya kiwango.
Habibu amesema ni vyema
mkulima akachukua tahadhari mapema, afahamu siku ngapi anaweza kuvuna
mazao yake baada ya kunyunyiza viwatilifu ili asiweze kupata madahara
baada ya kuvuna vinavyosababishwa na masalia ya viwatilifu katika mazao
Amesema kuwa TPRI ipo ili
kuthibitisha viwatilifu vinafanya kazi kama inavyokusudiwa , ili
kuhakikisha havileti madahara kwa binadamu,wanyama,na mimea ,sambamba na
kutokuvunja sheria ya uthibiti wa visumbufu vya mimea ya mwaka 1997
ambapo sheria hii imeainisha makosa na adhabu ikiwemo kifungo na faini.
"Kwa mfano kuuza
kiwatilifu ambacho hakina kibandiko cha maandishi ya kiswahili na
kiingereza ni kinyume cha sheria kipengele chake cha 20 ya sheria ya
usumbufu wa mimea faini yake ni shilingi za Kitanzania 2,000,000
"alisisitiza Habibu.
"Unajua viwatilifu ni
sumu ingawaje vinafaida kubwa,ndiyo maana tunasema tahadhari kubwa
ichukuliwe na vitumiwe kama sheria inavyovitaka,lakini mtu akikaidi na
kufanya atakavyo yeye sheria itachukua mkondo wake".alisema Habibu.
Aidha amesema kuwa (TPRI)
imekuwa ikitoa elimu kwa njia mbalimbali kwa kutoa mafunzo kwa
wadau,kwa kutoa huduma ya wima yaani kuwafuata wadau walipo,kupitia
ukaguzi wa viwatilifu kwa wauzaji na kwenye maonyesho mbalimbali.
Amewataka wadau wote wa
kilimo kutambua viwatilifu vilivyosajiliwa kwa kusoma maelezo
yaliyoandikwa kwa lugha ya kiswahili na kiingereza kwenye vibandiko,na
amewataka watambue kuwa wananchi wanalima mazao na jamii inakula mazao
.pia serikali inauza mazao nje ya nchi hivyo ni vyema viwatilifu
vikatumika vyema kama sheria inavyovitaka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni