SERIKALI YARIDHISHWA NA UWEKEZAJI KWENYE VIWANJA VYA NDEGE TBA

Na Ahmed Mahmoud Arusha SERIKALI imeridhishwa na utekekezaji wa miradi miwili ya maendeleo ya ujenzi wa Jengo la ghorofa kumi la nyumba za kuishii watumushi wa serikali lililopo mkabala na jengo la Uhamiaji mkoa pamoja na uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Arusha.. Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, ameyasema hayo ilipohitimisha ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi hiyo,iliyotanguliwa na Waziri huyo kufanya kikao na watumishi wa serikali kwenye ukumbi wa benki kuu. Kwenye mradi wa ujenzi wa Jengo la ghorofa kumi linalomilikiwa na linalijengwa na wakala wa majengo nchini TBA,Waitara,ameipongeza wakala huyo na kuagiza kuwa kipaumbele cha watu watakao ishi ndani ya jengo hilo iwe ni watumishi wa serikali. Alisema kukamilika kwa ujenzi wa Jengo hilo kutaongeza mapato ya serikali na uhitaji wa majengo ya kuishi watumushi ni mkubwa mno hivyo Jengo hilo litaiwezesha TBA,kujiendesha kibiashara . Alisema wizara imeshaagiza wastaafu ikiwemo wabunge waliomaliza muda wao kuondoka kwenye nyumbaza serikali zilizopo Dodoma ili kuwezesha watumishi wengine kupata nyumba za kuishi. Akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Arusha,Waziri Waitara,ameridhishwa na hatua za uboreshaji wa uwanja huo uliofanywa na mamlaka ya viwanja vya ndege nchini,na kusema kuwa serikali Imetoa fedha nyingi kwa ajilj ya miradi hiyo. Alisema kukamilika kwa ukarabati huo unahusisha kuongeza Urefu wa uwanja eneo la kurukia ndege kutaongeza ndege nyingi kutua uwanjani hapo na mapato nayo yataongezeka.kwani uwanja huo ni rafiki kwa watalii na wananchi wa mkoa wa Arusha Alisema jumla ya viwanja kumi na moja nchini vitafanyiwa marekebisho na uboreshaji katika bajeti ya mwaka huu na serikali sasa inafungua njia za uchumi kwa kuimarisha miundo mbinu ya barabara,reli,ndege na Mali kwa wizara hiyo ni wezeshi kufikia malengo ya kiuchumi. Kwa upande wake meneja wa uwanja wa ndege wa Arusha,Mhandisi Eliud Tesha,alisema mradi wa ukarabati na maboresho ya uwanja huo yanahusisha eneo la maegesho ya ndege na kuruka ,maegesho ya magari,eneo la kurukia ndege na miradi hiyo iliyotekelezwa ambayo imekamilika mwaka jana. Ameongeza kwamba mamlaka ya viwanja vya ndege nchini ina mpango wa kujenga jengo lingine la kisasa uwanjani hapo.la kufikia wageni kwa lengo la kuendelea kuongeza wigo mpana kwa abiria wanaofika kusafiri ndani ya uwanja huo.