WADAU WAAANZA KUJENGA UELEWA KUHUSU SIKU YA MAGONJWA YANAYOTOKEA KWA KUNDI DOGO LA JAMII

Wadau hao wakinyoosha mikono juu kuonesha umuhimu wa kuadhimishwa kwa siku hiyo ya Magonjwa Yanayotokea kwa kundi dogo la jamii ndani ya jamii.
Mratibu wa tukio hilo Bibi Sharifa Mbaraka akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye moja ya ukumbi wa hoteli ya Serena leo jijini Dar,Bi.Sharifa alisema kuwa tukio hilo limedhamiria kujumuisha  vyombo vya habari na wadau wengine ili kujenga uelewa kuhusu magonjwa hayo. 

“Yapo magonjwa tofauti yanayowasibu watu wachache takribani 7000 ambayo yameshabainishwa duniani hadi leo na Tanzania haiwezi kujitoa kwenye  hili. Hata hivyo watu wengi hapa Tanzania hawana uelewa  kuhusu magonjwa hayo”,alisema Bi Sharifa ambaye watoto wake wawili Ali Mohammed Kimara 5, na Nasreem Mohammed 3, wanasumbuliwa na magonjwa hayo.

Alifafanua kuwa kutokana na uzoefu wake, amepata msukumo  na kuamua kuwaunganisha wazazi, wagonjwa walio na magonjwa hayo na raia wenye mapenzi mema ili kujenga uelewa muhimu na kutoa wito kwa jamii kuchukua hatua.

Pichani wa pili kulia ni Mdau mkubwa wa sekta ya afya Monica Joseph kutoka Philips Medical Systems , akifafanua zaidi kuhusiana na huadhimishwa kwa Siku ya 'Rare Disease' Duniani ambayo inaadhimishwa leo.Monica amesema kuwa ni wakati mwafaka kwa Watanzania kuwa na tahadhari ya kuelewa kuhusu magonjwa hayo ili wanajamii waweze kufahamu mbinu za kuyadhibiti iwapo watayakuta ndani ya jamii. pichani kulia ni Dkt.Mariam Nooram kutoka hospital ya Aghakhan.
 
Kauli mbiu ya Siku ya Magonjwa Yanayotokea kwa kundi dogo la jamii Mwaka 2016 ni ‘Sauti za Wagonjwa’ na inamaanisha kutambua mchango muhimu unatolewa na wagonjwa katika kutaka mahitaji yao na kuchochea mabadiliko ambayo yataboresha maisha yao na masiha ya familia zao na maisha ya wale wanaowahudumia.

Kauli mbiu ya Siku ya Magonjwa yanayotokea kwa kundi dogo la wanajamii ambayo ni, “Ungana nasi kuzifanya sauti za waathirika zisikike” ikitaka jamii kwa jumla, wale wanaishi bila magonjwa hayo au wanaothirika nayo moja kwa moja kuungana na jamii ya waathirika katika kuelewa athari za magonjwa hayo. Watu wanaoishi na magonjwa hayo na familia zao mara kadhaa hutengwa. Jamii inaweza kuwaunganisha kutoka kwenye kutengwa huko. 

Lengo la jumla la Siku ya Magonjwa yanayotokea kwa kundi dogo la jamii ni kuhamasisha uelewa miongoni wa umma kwa jumla kuhusu magonwa hayo na athari zake kwa maisha ya wagonjwa ili kuyapa kipaumbele kwenye afya ya jamii ya Tanzania na kwenye bajeti ya serikali kupitia Wizara husika.

Professor Kareem Manji kutoka Muhimbili akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa Habari namna magonjwa hayo yanavyoisumbua jamii kwa kiasi kikubwa na pia uzoefu wake katika suala zima la kutoa matibabu,kushoto kwake ni Dkt Nurudin Lakhan ambaye pia alielezea namna ya magonjwa hayo  Yanayotokea kwa kundi dogo la jamii yanapaswa kuangaliwa upya ili kuitaka jamii kutambua kuwa magonjwa hayo yapo na yamekuwa yakiisumbua jamii kwa muda mrefu.
Bi.Monica Joseph kutoka Philips Medical Systems  alieleza mambo kadhaaa katika kupambana na magonjwa hayo,ameeleza kuwa ipo haja ya wadau wa sekta ya Afya na jamii kwa ujumla kuyafahamu magonjwa yasiyotambulika yapo katika jamii yetu na lazima tuchukue hatua za kushughulika nayo. Miongoni mwa hatua zinazopaswa kuchukuliwa ni pamoja na:
 
( a) Zifanyike juhudi za makusudi kuwapatia wataalam wa afya mafunzo maalum ya kutambua na kutibia magonjwa hayo,( b) Kuanzisha vitengo maalum vya kushughulikia magonjwa hayo hususan kwenye Hospitali za Rufaa. Vitengo hivyo havinabudi kuwa na vifaa mbalimbali vya kusaidia matibabu ya ugonjwa huo,(c) Uanzishwe mpango maalum wa kuwafanyia uchunguzi watoto wanaozaliwa ili kubaini kama wanao ugonjwa huo toka awali ili hatua zichukuliwe bila kuchelewa,(d) Serikali na wadau wengine wa Sekta ya Afya waangalie uwezekano wa kuwa na kampeni za kuelimisha umma juu ya ugonjwa huu kama inavyofanyika kwa magonjwa mengine kama cancer,malaria,kipindupindu,(e) Uangaliwe uwezekano wa kuanzisha shule maalum kwa ajili ya watoto wenye magonjwa yasiyotambulika.

Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

MAKAMU WA RAIS MSTAAFU DKT. BILAL AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA MASHINDANO YA KUTAFUTA WAWAKILISHI WA NCHI KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA QUR'AN TUKUFU.

Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu, Rajai Ayoub, aliyepata pointi 95 kwa upande wa Tajweed, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. . Kushoto ni Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar.
Makamu wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu, yaliyoandaliwa na Kamati Maalum chini ya Mwenyekiti wake Saleh Omary, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu, Abubakar Mohamed, aliyepata pointi 86 kwa upande wa washindani wa Juzuu 30, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. Kushoto ni Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar. 
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa pili wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu, Ibrahim Omary, aliyepata pointi 90 kwa upande wa Tajweed, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. Kushoto ni Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar.
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu, waliohudhuria mashindano hayo, wakimsikiliza Dkt. Bilal, wakati akihutubia. 
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu, waliohudhuria mashindano hayo, wakimsikiliza Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sl-had Mussa Salum, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, kufunga mashindano hayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo,Saleh Omary, akizungumza wakati wa mashindano hayo. 
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakati akiondoka kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu
Dua baada hafla hiyo


Mshiriki Rajab Juma, mshindi wa pili aliyepata pointi 78 katika Juzuu 30

Mshiriki Mbwana Dadi, mshindi wa tatu aliyepata pointi 75 katika Juzuu 30.
Mshindi wa kwanza katika juzuu 30, Abubakar Mohamed, aliyepata Pointi 86, akitafakari kabla ya kupanda jukwaani kushiriki.
Abubakar Mohamed, mshindi wa kwanza akishiriki....
Mshindi wa tatu kwa upande wa Tajweed, Ally Saleh, aliyeibuka na pointi 82
Mshindi wa kwanza kwa upande wa Tajweed, Rajai Ayoub, aliyeibuka na pointi 95.

Mshindi wa pili kwa upande wa Tajweed, Ibrahim Omaru, aliyeibuka na pointi 90.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA MTWARA

 Wamawake wakiwa wametandika khanga kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Februari 29, 2016.Waziri Mkuu, Kassim majaliwa alitembelea wodi hiyo na kukemea mtindo huo akiwataka wauguzi na waganga kutandika mashuka yahospitali ambayo alisema ana taarifa kuwa yapo ili kuepusha hatari ya wananwake hao kubeba magonjwa kupitia kahanga hizo watokapo hospitalini hapo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea hospitali ya Mkoa wa Mtwara Februari 29, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Halima Dendego na kulia Ni Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Shaibu Maarifa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waganga, Wauguzi na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakati alipoitembelea Februari 29, 2016.
 Baadhi ya Wauguzi na Madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao hospitalini hapo Februari 29, 2016. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim majliwa akitoa agizo la kusimamishwa kazi Daktari wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Fortunatus Namahala (kulia) baada ya kutajwa kuwa alidai rushwa ya sh.100, 000/= ili aweze kumtibu baba mzazi wa Tatu Abdallah (wapili kulia) wakati alipoitembelea hospitali hiyo Februari 29, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiagana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Shaibu Maarifa kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kurejea Dar es slaam Februari 29, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim majaliwa akitazama ngoma kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kuondoka kurejea Dar es salaam Februari 29, 2016.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA WARSHA YA PILI YA KIMATAIFA YA UNESCO MKOANI TANGA LEO.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
\Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika Firmin Matoko katikati na mwakilishi Mkaazi wa UNESCO Tanzania Zulmira Rodrigues kabla ya kufungua rasmi Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Balozi wa Korea kusini Nchini Geum-Young Song kabla ya kufungua rasmi Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Cheti kiongozi wa Spice kutoka Zanzibar ambae ni mmoja kati ya washiriki Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Cheti Judith Mwambela mmoja kati ya washiriki Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
(Picha na OMR)

Mke wa Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa WAMA asisitiza umuhimu wa Chama cha Girl Guide Tanzania Kuongeza Wanachama

 Mke wa Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa WAMA akisalimiana na Mama Othman Chande alipowasili katika Shule ya Sekondari Tambaza kuhudhuriaWorld Thinking Day iliyoandaliwa na Tanzania Girl Guide Association.
 Wanachama wa Girl Guide wakiwasili katika Shule ya Sekondari Tambaza  katika kusherekea World Thinking Day  ambao walipokelewa na Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete.
 Mama Salma Kikwete akiingia katika ukumbi wa Tambaza Sekondari akiwa na viongozi wa Girl Guide kushoto ni Mama Symphorosa Hangi, Kamishna Mkuu  na kulia ni Mama Matilda Balama na Mkuu wa Shule ya Tambaza.
 Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi  na baadhi ya wanafunzi Wanachama na viongozi wa  Girl Guide
 Mama Salma Kikwete akiangalia kazi za wakinamama wajasiriamali ambao walifanya maonyesho katika sherehe hizo.

PICHA NA YUSUPH BADI.

DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUFUNGWA KWA DUKA LA DAWA LA SHINE CARE PHARMACY LA TEMEKE KWA KUKIUKA UENDESHAKI WAKE.

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa kwa Duka la dawa za binadamu la Shine Care Pharmacy lililopo Temeke, baada ya kubainika kuendeshwa kinyume cha sharia ikiwemo kutokuwa na kibali cha uendeshaji na mfamasia husika.

Dk. Kigwangalla ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Mfamasia Mkuu wa Serikali pamoja na msajili wa Baraza la famasia nchini na maafisa wengine, ambapo katika tukio hilo mapema leo Februari 29.2016, walikuta madawa mbalimbali yaliyokwisha muda wake na yale ambayo hayatakiwi kuuzwa katika duka kama hilo.

Aidha, Dk. Kigwangalla akitoa agizo la kufungwa kwa duka hilo, ameagiza kuchukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa Mahakamani mara moja il iwe fundishi na kwa maduka mengine yenye kufanya hivyo.

Kwa upande wake, Mfamasia wa Serikali, Bw. Henry Irunde amebainisha kuwa, dawa hiza za binadamu zilizokutwa hazifai kuuzwa katika maduka hayo na pia duka ambalo linaendeshwa bila kuwa na Mfamasia ni kinyume na sharia kwani watumiaji wakitumia dawa bila kuwa na maelezo ya kutosha kutoka kwa mtaalam wa dawa zinaweza kusababisha usugu kwa mwili wa binadamu n ahata kumsababishia matatizo.

Duka hilo la dawa ambalo lipo hatua chacche kutoka Hospitali ya Temeke, ni miongoni mwa maduka makubwa ya dawa za binadamu ambapo pia wachunguzi ha wa madawa ya binadamu walibaini kuwa milango mingi zaidi kinyume na ile inayotakiwa kuwa kwa maduka ya dawa hali ambayo walitilia mashaka huenda vitendo vingine vya kutoa huduma vinatumika licha ya kuwa milango hiyo ilifungwa kwa kile kilichoelezwa kuwa wahusika hawakuwapo.

Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, zoezi hilo la kukagua maduka ya dawa ni la nchi nzima na watazunguka nchi nzima kufanya ukaguzi huo bila kutoa taarifa hivyo kwa yeyote atakaekutwa anaendesha kinyume cha sharia atachukuliwa hatua stahiki.



Tazama  tv, Kuona video hiyo hapa: 
Imeandaliwa na Andrew Chal.
Mmoja wa maafisa wa TFDA, akikagua dawa katika duka hilo
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akiwaonyesha waandishi wa habari cheti cha Famasia kilichoisha muda wake huku akiendelea na biashara yake hiyo kinyume na sheria.
Baadhi ya maafisa walioambatana na Naibu Waziri wa Afya. Dk Kigwangalla wakimsikiliza kwa makini, Dk. Kigwangalla (hayupo pichani) wakati wa tukio hilo.
Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akiongea kwa njia ya simu na mmiliki wa duka hilo la Shine Pharmacy , Abraham Mathayo...ambaye alieleza kuwa yupo Mkuranga, hivyo waliamua kuongea naye kwa njia ya simu kwa nini anaendesha duka bila ya kutokuwa na vibali.
Mfamasia Mkuu wa Serikali Henri Irunde, akitoa taarifa yake ya ukaguzi katika duka hilo kwa wanahabari na Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani).
Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo ya kufungwa kwa duka hilo.
Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla akitoka katika duka hilo la dawa baada ya kuagiza kulifunga.
(Picha zote na Andrew Chale.)