Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa
Habari leo jijini Dar es salaam kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi na
ukarabati wa barabara za Halmashauri nchini unaotekelezwa kwa
ushirikiano na shirika la Maendeleo la Japan ( JICA) mradi unaolenga
kuwajengea uwezo wahandisi wa Halmashauri na Mikoa katika kusimamia na
kukarabati barabara zilizopo katika maeneo yao kwa kushirikiana na
wananchi.
Mhandisi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Chamwino Godwin Mpinzile akieleza kwa waandishi wa Habari
kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara na ukarabati katika
Halmashauri hiyo unaofadhiliwa na JICA ukilenga kuwashirikisha wananchi
katika ujenzi na utunzaji wa barabara hizo ili ziweze kudumu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe akimpongeza Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la maendeleo la Japan (JICA) hapa nchini bw. Nagase Toshio kwa
ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Japan hali iliyochangia
kufanikiwa miradi ya ujenzi wa barabara katika halmashauri mbalimbali
hapa nchini inayofadhiliwa na shirika hilo.
Muwakilishi Mkazi wa Shirika la
maendeleo la Japan (JICA) bw. Nagase Toshio akifafanua kuhusu
ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Japan katika
kutekeleza mradi huo unaolenga kujenga uwezo kwa wahandisi wa
Halmashauri hapa nchini ili waweze kuwashirikisha wananchi katika miradi
ya barabara inayotekelezwa ili waweze kujiletea maendeleo .
Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Iringa bw. leopold Runji akitoa ushuhuda wa namna halmashauri hiyo
ilivyonufaika na mradi wa ujenzi na ukarabati wa barabara unaotekelezwa
katika halmashauri hiyo kwa ufadhili wa shirika la JICA.(Picha zote na
frank Mvungi-Maelezo)
………………………………………………………………………………………………………….
Frank Mvungi-MAELEZO
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
TAMISEMI bw. Mussa Iyombe amewataka wananchi kutunza barabara
zinazojengwa na Serikali kwa kushirikiana na wafadhili katika
Halmashauri zote hapa nchini.
Akizungumza leo Jijini Dar es
salaam katika hafla fupi ya kupokea ripoti ya utekelezaji wa mradi wa
Ujenzi na ukarabati wa barabara za halmashauri nchini Iyombi
amebainisha kuwa mradi huo umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la
Japan (JICA) .
“Mradi huu unatekelezwa katika Halmashauri za Iringa,Mufindi,Chamwino na Kondoa” alisisitiza Iyombe.
Akifafanunua kuhusu utekelezaji
wa mradi huo Iyombe amebainisha kuwa unadhamiria kujenga uwezo kwa
wahandisi wa Mikoa na Halmashauri hapa nchini ili waweze kushirikiana
na wananchi katika kujenga na kulinda miundo mbinu hiyo kwa maslahi ya
Taifa.
Aidha Iyombi amewata
wakurugenzi wa Halmashauri ambazo mradi huo unatekelezwa kutunza
barabara hizo ili zilete matokeo yaliyokusudiwa.
Akizungumzia ushirikiano mzuri
uliopo kati ya Japan na Tanzania Iyombe amesema kuwa maeneo ambayo
Tanzania imekuwa ikipata ufadhili kutoka Japan ni Sekta ya
Kilimo,Viwanda,Uimarishaji wa Utawala bora.
Kwa upande wake mwakilishi mkazi
wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) bw. Nagase Toshio amesema kuwa
Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika
kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mradi wa Ujenzi na Ukarabati wa
barabara katika Halmashauri hapa nchini unatekelezwa kwa awamu ambapo
awamu ya kwanza imekamilika katika Halmashauri za Chamwino na Iringa na
awamu ya pili imekamilika katika Halmashauri za Kondoa na Mufindi ambazo
ripoti ya utekelezaji wake iliwasilishwa leo katika mkutano wa siku
moja ulifanyika Jijini Dar es salaam ukilenga kufanya tathmini ya
utekelezaji kabla ya kuanza kwa awamu ya tatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni