Hali ya hisia kali ilitawala katika
Ikulu ya Marekani baada ya kibibi cha miaka 106 kutinga Ikulu kikiwa
na furaha tele huku kikicheza na rais Barack Obama na mkewe Michelle,
licha ya kuwa na umri mkubwa.
Kikongwe huyo machachari alipaza
sauti kwa furaha mara tu ya kuingia Ikulu ya Marekani huku
akimsalimia rais Obama na kisha kusema alifikiri asingewahi kuingia
Ikulu katika maisha yake.
Bibi Virginia McLaurin alionekana
kutimiza ndoto yake ya muda mrefu aliyokuwa akiiota alijawa na furaha
isiyo na kifani na hakusita kusema kuwa anafuraha kushuhudia rais
mweusi akiiongoza Marekani.
Bibi Virginia McLaurin akicheza muziki na Michelle Obama
Rais Obama akiangua kicheko wakati akicheza na bibi huyo pamoja na mkewe
Michelle Obama akimkumbatia kwa furaha Bibi Virginia McLaurin
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni