Baadhi ya waandaji wa Filamu
nchini wakifuatilia mada katika kikao kilichowakutanisha waandaaji wa
Filamu,Bodi ya Filamu, COSOTA na Kampuniya BORA PAMOJA LTD ili kujadili
bidhaa ya Kampuni hiyo inayojulikana kwa jina la Tazama Kidigitali
ambayo inatoa fursa kwa watengenezaji na wamiliki wa Filamu kuusambaza
kazi zao kupitia mfumo wa kidigitali leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akizungumza wakati wa kikao cha wasanii na
Kampuni ya Bora Pamoja Ltd ili kujadili bidhaa yao ya Tazama Kidigitali
ambayo inatoa fursa kwa watengenezaji na wamiliki wa Filamu nchini
kuusambaza Filamu zao kupitia mfumo wa kidigitali leo jijini Dar es
Salaam.A
fisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
BORA PAMOJA LTD Bi. Beatrice Pugwe akizungumza katika kikao
kilichowakutanisha waandaaji wa Filamu na Kampuni yao ili kujadili
bidhaa ya Kampuni hiyo inayojulikana kwa jina la Tazama Kidigitali
ambayo inatoa fursa kwa watengenezaji na wamiliki wa Filamu kuusambaza
kazi zao kupitia mfumo wa kidigitali leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa
Kampuni ya BORA PAMOJA LTD Bw. Mwanga Mwakibete akizungumza katika kikao
kilichowakutanisha waandaaji wa Filamu na Kampuni yao ili kujadili
bidhaa ya Kampuni hiyo inayojulikana kwa jina la Tazama Kidigitali
ambayo inatoa fursa kwa watengenezaji na wamiliki wa Filamu kuusambaza
kazi zao kupitia mfumo wa kidigitali leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Filamu
Tanzania (TAFFA) Bw. Simon Mwakifamba akichangia mada katika kikao
kilichowakutanisha waandaaji wa Filamu,Bodi ya Filamu, COSOTA na
Kampuniya BORA PAMOJA LTD ili kujadili bidhaa ya Kampuni hiyo
inayojulikana kwa jina la Tazama Kidigitali ambayo inatoa fursa kwa
watengenezaji na wamiliki wa Filamu kuusambaza kazi zao kupitia mfumo wa
kidigitali leo jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………………………………
Na Shamimu Nyaki.
“Mmebuni wazo zuri lenye tija kwa
waandaaji wa waongozaji wetu ambapo naamini itawaletea manufaa katika
kazi zao wanazotengeza ili ziwe na faida kwao kwa kujitangaza kimataifa
pamoja na kukuza kipato chao.’’ Alisema Bi Joyce.
Kampuni ya Bora Pamoja Limited
imeanzisha mfumo mpya wa usambazaji wa Filamu za hapa nchini kwa njia
ya kidigitali ili kuweza kujitangaza kimataifa.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
Salaamu na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bi Beatrice Mpungwe alipokuwa
anazugumza na waandaaji pamoja na wasambazaji wa filamu za hapa nchini
ambapo amesema kampuni hiyo itawawezesha kukodisha filamu zao kwa
wakati wowote wanaota pamoja na kujitangaza kimataifa.
Bi Beatrice ameongeza kuwa
kampuni hiyo ina nia ya kutangaza na kusambaza filamu kwa njia ambayo
inaendana na wakati uliopo kwa kukuza kazi za watengenezaji na
wasambazaji wa filamu kwa ajili ya kuhifandhi kumbukumbu ya nchi na
vizazi vijavyo.
‘’Mpango huu una nia ya
kubadilisha jinsi tunavyoweza kutengeneza filamu zetu ziwe katika
kiwango cha kimataifa kuanzia uandishi,uigizaji, uongozaji na
utengenezaji”.Alisema Bi Beatrice.
Aidha Katibu Mtendaji wa Bodi ya
Filamu nchini Bi Joyce Fissoo ameipongeza Kampuni hiyo na kuwashauri
waandaaji na wasambazaji wote kujiunga na mfumo huo kwakua una lengo la
kubadilisha uchumi na soko la kazi zao.
Amesema kuwa Mfumo huo
utawawezesha kujua ni idadi ngapi ya filamu zimeingia sokoni ambazo
tayari zimeshafanyiwa uhakiki na Bodi ya Filamu ili kuweza kufikia lengo
la kuinua tasnia ya filamu hapa nchini.
“Mmebuni wazo zuri lenye tija kwa
waandaaji wa waongozaji wetu ambapo naamini itawaletea manufaa katika
kazi zao wanazotengeneza ili ziwe na faida kwao kwa kujitangaza
kimataifa pamoja na kukuza kipato chao.’’ Alisema Bi Joyce.
Hata hivyo mfumo huu utashawishi
wawekezaji kutoka sehemu tofauti ndani na nje ya nchi,kuwekeza katika
vitendea kazi thabiti vitakavyosaidia katika kutengeneza kazi zenye
ufanisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni