Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu Bw.
Eric Shitindi akizungumza na vijana (hawapo pichani) alipokuwa
akifungua kikao cha wadau wa maendeleo ya vijana katika kuchangia
uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akizungumza wakati wa kikao cha
wadau wa maendeleo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za
uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji
Bw. Patrick Kipangula (aliyesimama) akitoa mada kwa wadau wa maendeleo
ya vijana wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji
wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa
maendeleo ya vijana akichangia mada wakati wa kikao cha kuchangia
uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini
Dar es Salaam.
Wawakilishi
kutoka Mamlaka mbalimbali za Serikali, Asasi za kiraia, Vyama vya
siasa, Taasisi za kidini, Vijana wenye ulemavu, Shule za sekondari na
Shule za msingi wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikiendelea
wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza
la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu Bw.
Eric Shitindi (watatu kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na
vijana wenye ulemavu wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za
uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam. Wapili
kulia (waliokaa) ni Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi,
wapili kushoto ni Mwenyekiti wa kikao Bw. Godwin Kunambi, na wanne kulia
(waliosimama) ni Mkurugenzi msaidizi Vijana Bibi. Ester Riwa
Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo
Na; Genofeva Matemu – Maelezo
SERIKALI
imedhamiria kuhakikisha kuwa vijana wanakuwa na chombo chao chenye
kujali utaifa, uzalendo na maslai bila kujali itikadi za kisiasa,
kidini, rangi, hali za kiuchumi, jinsia na maumbile kwa kuandaa kanuni
zitakazolifanya Baraza la Vijana Taifa kuwa huru na lenye haki.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na
watu wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi alipokuwa akifungua kikao cha wadau
wa maendeleeo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za
uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
“Nimuhimu
kuunda Baraza kisheria litakalokuwa na uwakilishi wa vijana wa makundi
yote ili liweze kutumika katika kuleta umoja na mshikamano wa kitaifa”
alisema Bw. Shitindi
Aidha
Bw. Shitindi amelipongeza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kuweza kutunga sheria Na. 12 ya mwaka 2015 ya Baraza la Vijana Taifa
ambalo litaleta maendeleo ya vijana na nchi kwa ujumla.
Akizungumza
katika kikao hicho mwenyekiti aliyeteuliwa kuongoza mjadala huo Bw.
Godwin Kunambi amesema kuwa Vijana takribani 120 wamepata fursa adhimu
ya kushiriki katika uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana
Taifa hivyo kuwataka vijana hao kujadili mambo ya msingi
yatakayowawezesha wananchi wa Tanzania hususani vijana kutatua kero zao
kupitia Baraza hilo.
Naye
mwakilishi kutoka kundi la watu wenye ulemavu Bw. Gaston Hemed Mcheka
ameipongeza Serikali kutoa nafasi kwa kundi la watu wenye ulemavu kuwa
na uwakilishi kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa pindi Baraza la Vijana
Taifa litakapoanza ambapo kundi hilo litatumia nafasi hiyo kutatua
changamoto zinazowakabili.
Kikao
cha wadau wa maendeleo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za
uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa kimeshirikisha takribani vijana
120 kutoka Mamlaka mbalimbali za Serikali, Asasi za kiraia, Vyama vya
siasa vilivyosajiliwa, Taasisi za kidini, Vijana wenye ulemavu, Shule
za Sekondari pamoja na Shule za msingi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni