Vita ya Kupambaza na Uwepo wa Magugu Maji katika Maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria, bado haijazaa matunda Chanya.
Suala
la kupambana na magugu maji katika ziwa hilo bado ni changamoto, licha
ya kuwepo kwa Miradi mbalimbali ikiwemo ile ya Uhifadhi wa Mazingira ya
Bonde la Ziwa Victoria (LIVEMPT I & II) iliyolenga kuokoa uwepo wa
Ziwa Victoria ambayo pia ililenga kupambana na magugu maji.
Mara
kadhaa huduma za usafirishaji katika Kivuko cha Busisi, Wilaya ya
Misungwi Mkoani Mwanza, zimekuwa zikitatizwa na uwepo wa Magugu maji
ambayo hutanda katika eneo la ferry la kivuko.
Usumbufu
kama huo unahofiwa huenda ukajitokeza katika eneo la Kamanga Ferry
Jijini Mwanza, baada ya Magugu Maji kugonga hodi na kuanza kutanda
katika eneo hilo.
Kumbuka
Magugu maji yanaweza kutambaa kutoka eneo moja hadi jingine kulingana
na upepo unavyovuma na yanaweza kuleta athari ya usafirishaji majini
ikiwa chombo cha usafiri (Meli/Ferry) kitanasa katika Magugu maji.
Suala
kubwa ni kuhakikisha mapambazo zaidi dhidi ya magugu maji yanaendelea
ikiwemo kuvitumia vikundi vya Kusimamia Rasilimali za Uvuvi katika Ziwa
Victoria (Beach Management Unit-BMU) ambavyo mara moja moja pale
vinapowezeshwa, vimekuwa vikifanya shughuli ya kutoa magugu maji Ziwani.
Hata
hivyo jitihada za vikundi hivyo zimekuwa zikikwama kuleta suluhisho
maana magugu maji yanapotolewa majini, ni vyema yakachomwa moto jambo
ambalo huwa ni nadra kufanyika na matokeo yake magugu maji hayo hurudi
ziwani kwa njia moja ama nyingine, ikiwemo kwa njia ya shughuli za
kilimo katika maeneo ya kandokando mwa ziwa Victoria.
Shughuli za Kupambana na Magugu Maji zikifanyika eneo la Nera Jijini Mwanza mwishoni mwa Mwaka jana
Imeandaliwa na George
Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni