Mratibu
 wa Kituo cha usuluishi cha TAMWA, Bi. Gladness Hemedi Munuo akizungumza
 mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati walipokuwa 
wakilaani vikali ucheleweshwaji na upotoshaji wa kesi za vitendo vya 
ukatili. 
Mtoto akitoa ushaidi ni kwa jinsi gani alivyofanyiwa kitendo cha ukatili wa kijinsia. 
Mwanasheria
 wa TAWLA, Mary Richard (wa kwanza kulia) akizungumza ni kwa jinsi gani 
wanavyowasaidia wanawake wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia 
leo katika mkutano na waandishi wa habari leo. 
CHAMA 
cha Wanahabari wanawake nchini Tanzania(TAMWA) kimelaani vikali 
ucheleweshwaji na upotoshwaji ushahidi wa kesi za vitendo vya ukatili wa
 kijinsia hasa ubakaji na ulawiti katika ngazi ya mahakama, polisi na 
baadhi ya madaktari hospitalini. Hali hiyo imekuja baada ya TAMWA 
kubaini kesi sitini na mbili (62) za ubakaji zimeshindwa kutolewa hukumu
 au uamuzi na mahakama mbalimbali jijini Dar es Salaam katika kipindi 
cha mwaka 2014 hadi 2015. 
Akizungumza
 na waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga
 amesema kati ya kesi 63 za ubakaji, ni kesi moja tu mtuhumiwa 
amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kesi arobaini na tatu (43) bado 
ziko mahakamani, kesi kumi na saba (17) zimeshindwa kufika mahakamani 
ambapo kesi mbili zimefutwa kwa kukosa ushahidi. 
Pia 
aliongezea kwa kusema kuwa uongozi wa TAMWA umesikitishwa kuona kesi 
hizo zikicheleweshwa na vyombo mbalimbali vya serikali ikiwemo jeshi la 
polisi na mahakama. Na kuna baadhi ya viongozi wanapokea rushwa ili 
kuzima kesi za watoto wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia, pia baadhi ya 
polisi wamekuwa wakishindwa kutoa ushirikiano kwa mlalamikaji ambapo 
wanatoa maneno ya vitisho na kupelekea mlalamikaji kukosa ujasiri wa 
kuhifadhi na kutetea kesi yake na wakati mwingine mama mzazi anaandikwa 
kama mlalamikaji badala ya mtoto mwenyewe aliyefanyiwa ukatili huo. 
Pia 
wameunga mkono tamko la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliposema wakati wa siku ya sheria 
duniani kuwa "Kila Hakimu wa Mahakama anapaswa kuhukumu kesi si chini ya
 260 kwa kila mwaka na kwa haki", Hivyo basi wao kama TAMWA wanaamini 
ndani ya mwaka huu Mahakama hapa nchini zitafanya kazi yao kiweledi ili 
kuweza kupunguza ukatili wanaofanyiwa watoto wa kike.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni