Mtafiti
Kiongozi Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus
Nyange (katikati), akizungumza na wakulima wa Wilaya ya Rorya Mkoani
Mara katika mafunzo ya siku moja kwa wakulima hao ya kutumia simu
kupashana habari za kilimo na kujua changamoto zinazo wakabili. Kulia ni
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia za Kilimo Afrika (OFAB), Daniel
Otunge na kushoto ni Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania
(OFAB), Dk.Emmarold Mneney.
Maofisa Ugani wa Wilaya ya Rorya wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Rorya, Dominick Ndentabura akizungumza na wakulima hao kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
Mkulima
Sophia Charles kutoka Kijiji cha Roche akizungumzia changamoto ya
ukosefu wa soko la zao la mhogo ambapo wanategemea zaidi soko nchini
Kenya.
Mkulima Charles Ruola akizungumzia changamoto ya kilimo cha mahindi.
Mkulima
wa Kijiji cha Kowaki kilichopo Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Elias
Kaseno akizungumzia changamoto ya kilimo cha muhogo na mahindi mbele ya
watafiti kutoka Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB) na Watafiti kutoka Tume
ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), waliopo wilayani humo jana
kujua changamoto mbalimbali za wakulima na kutoa mafunzo ya matumizi ya
Bioteknolojia katika kilimo.
Mratibu
wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi akielekeza
jinsi ya kupiga simu wakati akiendesha mafunzo hayo kwa wakulima.
Wakulima wakiwa kwenye mafunzo.
Wakulima wakiwa mafunzo hayo.
Wakulima wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Jengo la Halmshauri ya Wilaya ya Rorya.
Shamba
la muhogo lililoshambuliwa na ugonjwa wa batobato lililopo jirani na
jengo la Halmshauri ya Rorya ambapo wapo wataalamu wa kilimo.
…………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
KATIKA
hali isiyotegemewa shamba lenye ukubwa wa ekari moja la zao la muhogo
lililopo nyuma ya Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara
ambapo ofisi ya wilaya ya kilimo ipo halipo katika matunzo ya kilaalamu
ambapo mwandishi wa habari hii ambaye yupo katika ziara ya kilimo na
watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech)
alitembelea.
Mwandishi wa habari hii
alidhani kuwa shamba hilo la muhogo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia
wakulima kuhusu ugonjwa unaoshambulia zao hilo ujulikanao kama batobato
na athari zake kumbe ni shamba la mkulima ambalo limekosa huduma za
ugani licha ya maofisa ugani kuwepo mita chache ya eneo hilo.
Kutokana na hali hiyo inapaswa wakulima wa namna hiyo kupata huduma za kilimo kutoka maeneo mengine kutokana na maofisa ugani hao kushindwa kutoa elimu ambapo shamba hilo limekuwa ni chanzo cha kueneza ugonjwa huo katika maeneo mengine.
Akizungumza katika mafunzo ya matumizi ya simu katika kilimo kwa wakulima wa wilaya ya Rorya Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi alisema mafunzo hayo ya siku moja yatawasaidia wakulima kupashana habari za kilimo na changamoto zao.
“OFAB imeleta mafunzo haya kwa wakulima ambao ni wadau wetu ili waweze kupashana habari za kilimo, changamoto zinazo wakabili na kutafuta masoko ya mazao yao kwa njia ya simu badala ya kutumia simu hizo kupigiana kwa mambo ya kawaida” alisema Nyinondi.
Alisema kupitia mafunzo hayo wakulima hao wataweza kushirikiana na mitandao mingine ya kijamii ili kutatua changamoto zao za kilimo zikiwemo za wadudu waharibifu wa mazao, ukame na nyinginezo.
Alisema washiriki wa mafunzo hayo walikuwa ni 20 kutoka katika wilaya hiyo na kuwa shirikisha wataalamu wa kilimo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni