Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
………………………………………………………………………………………………….
Mahmoud Ahmad Arusha
Wajasiriamali kote nchini
wakiwamo pia wakulima na wafugaji nchini wametakiwa kuchangamkia fursa
ya mikopo ya vifaa ikiwemo trekta na mashine mbali mbali za kilimo na
ufugaji sambamba na
vifaa mbali mbali lengo likiwa ni kukuza kipato kwa wananchi.
vifaa mbali mbali lengo likiwa ni kukuza kipato kwa wananchi.
Akizungumza na waanahabari meneja
mikopo wa kampuni ya Wasambazaji wa vifaa kutoa mikopo kwa
wajasiriamali bila dhamana yeyote (EFTA)yenye makao makuu yake Mjini
Moshi mkoani Kilimanjaro Peter Temu amesema kuwa wanawakaribisha
wananchi kwenye maonyesho hayo ya siku tatu yakatayofanyika mkoani hapa.
Amesema kuwa kwenye maonyesho
hayo zaidi ya wauzaji na wasambazaji wa mashine 25 watakuwa wakionyesha
bihdaa na mashine walizonazo kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wananchi
watakaoudhuria ili wajue matumizi bora ya mashine aina,mashine
halisi,waranti na mabo mengine mbali mbali bila ya kiingilio.
Alisema kuwa mbali na maonyesho
hayo ya EFTA pia wamejianda kuwafanya watembeleaji wa mabanda ya
maonyesho hayo kuona na kupata mambo mengi ya ziada ikiwemo kupata
semina na mafunzo kwa wajasiriamali toka kwa wataalamu mbali mbali bila
malipo.
“Mafunzo haya yatatolewa bure na
wataalamu wenye uzoefu na masuala ya ujasiriamali na kilimo ili wakulima
na wajasiriamali wapate faida ya shughili wanazofanya kama kuongeza
thamani katika bidhaa wanazozalisha na vifungashio vya kilimo na
viwandani”alisema Temu
Alisema hiyo itakuwa fursa muhimu
nay a kipekee kwa watanzania watakaobahatika kufika kwenye viwanja vya
makumbusho kwa siku tatu kuanzia Alhamisi hadi yatakapofungwa jumamosi
huku wakitarajia wakazi wengi kutoka mikoa ya kaskazini ikiwemo
Kilimanjaro,Tanga,Arusha na Manyara kuchangamkia na kufika kukutana na
wauzaji na was am,bazaji hawa huku wakijua kuwa EFTA LTD inafanya nn kwa
ajili yao katika shughuli nzima ya utoaji wa mikopo bila dhamana na
kutoa huduma ya mikopo moja kwa moja kwa wajasiriamali na wakulima wote
watakaofika katika maonyesho hayo.
“Tunaposema mashine za kila Aina
tunamaanisha anazohitaji mteja na sio kuwa tunamchagulia mteja,mfano
mashine na vifaa vya kilimo,mashine za kufyatulia matofali,mashine za
kukamulia alizeti vifaa vya maabara mashine za kutengeneza chakula cha
mifugo na kutotolea vifaranga pamoja kilimo cha umwagiliaji na green
house na nyingine nyingi’’Alisema Temu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni