Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kaskazini. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kaskazini. Onyesha machapisho yote

MUWSA YAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI ZA KUTOA ELIMU BURE,YACHANGIA MATOFALI 2300 KWA AJILI YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA WILAYANI HAI.

Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa tofali 2300 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,Joyce Msiru akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa wakati wa kukabidhi madawati kwa ajili ya shule ya msingi Msamadi.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiongozana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA),Joyce Msiru wakitizama ujenzi wa madarasa matatu unaoendelea katika shule ya msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akipeana mkono na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msamadi ,Seseama Bayo mara baada ya kupokea matofali 2300 yaliyotolewa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA).


Mafundi wakishusha tofali zilizotolewa na MUWSA kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) Joyce Msiru akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa .wengine ni watumishi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa madarasa hayo.
Jengo jipya lenye madarasa mawili katika shule ya msingi Msamadi ambalo kwa kiasi kukamilika kwake kutasaidia kupunguza changamoto ya vyumba vya madarasa shuleni hapo.


Moja ya madarasa yaliyopo shuleni hapo kama linavyoonekana ambapo wanafunzi wamekuwa wakikaa chumba kimoja kwa idadi kubwa kuliko uwezo wa darasa.
 
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.

SEREKALI YATAKIWA KUANGALIA KWA MAKINI BAJETI YAO YA MWAKA WA FEDHA 2016/2017 KWA KUANGALIA ZAIDI SEKTA YA AFYA PAMOJA NA ELIMU

Na Mahmoud Ahmad,Arusha
BAADHI ya wananchi wa mkoani Arusha wameiomba serikali kuhakikisha
bajeti ijayo ya mwaka wa fedha inawaangalia kwa jicho la pili wananchi
wenye kipato cha chini ambao hawana uwezo wa kukidhi baadhi ya
mahitaji yao kwa kupunguza bei ya bidhaa ili kupunguza makali ya
maisha
 Serikali ya awamu ya tano kama  itaweza kupunguza baadhi ya
kodi katika mahitaji muhimu basi maisha ya wananchi wenye kipato cha
chini yataweza kuboreka na hivyo umaskini utapungua kwa kiwango
kikubwa tofauti na sasa.

Hayo yameelezwa na wananchi wa jiji la Arusha wakati wakiongea na
  Na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na bajeti ijayo ya serikali ambapo wamedai
bajeti hiyo inatakiwa kulenga kwenye vipaumbele maalumu ambavyo
vinagusa maisha ya wananchi ya kila siku na sio ya kulenga watu wenye
vipato vya juu tu

  Kwa upande wake mmoja wa wananchi  hao aliyejitambulisha kwa jina La Enjo John alisema kuwa kwa sasa maisha ya
watanzania hususani wenye kipato cha chini wanashindwa kumudu milo
mitatu kwa siku kutokana na baadhi ya bidhaa kuuzwa kwa bei ya juu
sana kitu ambacho kinachangia kuongeza kiwango cha umaskini na lishe
duni kwenye baadhi ya familia.

alitolea mfano wa bidhaa za sukari, mchele, mafuta, nguo ambapo
kutokana na kipato ambacho wanapata baadhi ya watanzania kinasababisha
wakose mahitaji hayo ambayo ni muhimu kwa siku.

“bajeti hiyo inatakiwa itoe vipaumbele kwenye chakula kodi zisizo na
maana ziondolewe kabisa chakula kiwe na uhakika na kama itakuwa hivyo
watu wengi watapata fursa ya kuwa na afya njema na kisha kulitumika
taifa letu”aliongeza Emanulel Peter

  Aliongeza kuwa bajeti ya serikali
inatakiwa kutoa vipaumbele kwenye sekta ya elimu,afya,pamoja na
uwekezaji wa ndani

Alisema   Kwa upande wa  sekta ya afya kunatakiwa kuwe na huduma bora
ambapo huduma hizo ni pamoja na wingi wa vituo vya afya, lakini pia
hata dawa ,nyumba za watumishi, pamoja na huduma ya mama na mtoto kwa
kuwa kwa maeneo ya vijijini wanawake wengi wanafariki wakati wakiwa
wanajifungua.

Kwa upande wa wanawake wa jiji la Arusha walisema kuwa bajeti
inatakiwa ikidhi mahitaji muhimu hususani ya elimu kwani asilimia
kubwa ya wanawake wanabeba majukumu ya kusomesha familia zao.

Mmoja wa wanawake hao,ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari Nasholi
  Aggness Limo alisema kuwa bajeti inayokuja ilenge kuboresha
mazingira ya walimu ikiwepo nyumba za kuishi ,kuboreshewa maslahi
pamoja na wanafunzi kuongezewa vitabu vya kiada na ziada kwani
vimekuwa ni changamoto kubwa sana mashuleni.

Nae mmoja wa   askari usalama alisema kuwa ni vema bajeti inayokuja
ikatoa vipaumbele kwa maaskari kuboroshewa mishahara ,kuongezewa
vitendea kazi vya kisasa na kujengewa nyumba za kuishi kwani baadhi ya
maaskari wanaishi nyumba ambazo hazina hadhi na wao.

DC ARUSHA ATAPELIWA MILINI 10 NA WEZI WA MTANDAO

 mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu akiwa ofisini kwake anaongea na waaandishi jinsi alivyotapelewa shilingi milioni kumi na wezi wa mitandao
Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu akiwa anaonyesha ujumbe mfupia wa maneno ambao matapeli hao walikuwa wanatuma kwa watu
Na Mahmoud Ahmad ,Arusha.


Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu ameibiwa kiasi cha shilingi milioni 10 na wezi wa mtandao ambao waliteka mawasiliano yake ya simu za mkononi kwa muda wa saa 3 na kutumia namba hizo kuomba fedha kwa watu wa karibu na kiongozi huyo.


Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake ,Nkulu amesema kuwa jana majira ya saa 10:00 alasiri simu zake zilikua hazipatikani hewani mpaka majira ya saa 3:00  usiku ndipo aliposhtuka na kuanza kufuatilia na kugundua kuwa mawasiliano yake yalitekwa kwa muda.


Mkuu huyo wa Wilaya amelaani  vitendo vya wizi wa mtandao vinavyofanywa na watu wenye nia ovu huku akiwataka wananchi na wamiliki wa makampuni ya simu kuwa makini juu ya wizi huo wa kimtandao ambao umeshamiri miaka ya hivi karibuni.


Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa Yoitham Ndembeka ambaye alitumiwa ujumbe wa kumtaka atume fedha kupitia namba ya mkuu huyo wa wilaya  amesema kuwa baada ya kusumbuliwa na matapeli hao ambao hawakutaka kupokea simu aliamua kuachana nao huku akitafuta namna ya kuonana ana kwa ana na Mkuu huyo wa Wilaya.


Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel kanda ya Kaskazini alipotafutwa kujibu madai hayo simu yake haikupatikana hewani.


Wizi wa mitandao umeshamiri na kushika kasi hasa katika kipindi hiki ambacho teknolojia imekua kwa kiasi kikubwa ,hivyo makapuni ya simu,mamlaka za kusimamia teknolojia ya mawasiliano TCRA pamoja na polisi wanapaswa kuchukua hatua kupambana na uhalifu huo.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NORWAY ATEMBELEA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA



Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Dk Richard Masika(kushoto)akimwongoza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen kuwasilimia wafanyakazi wa taasisi hiyo katika ziara yake ,Norway ni moja ya nchi zinazosaidia sekta ya elimu ya ufundi nchini. 

Ujumbe uliongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen kutoka Norway na maafisa kutoka ubalozi wao nchini wakisalimiana na wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi Arusha. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen (kulia)akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhil Nkurlu(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Richard Masika. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen na ujumbe wake wakipata maelezo ya mfano wa kuzalisha umeme unaotokana na chanzo kidogo cha maji. 
Mmoja wa wanafunzi anayesoma katika Chuo hicho akimpa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen maelezo kuhusiana na kozi yake. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo.

WAZAZI WAOMBA SEREKALI KUCHUNGUZA KWANINI WATOTO WAO WANAFELI SANA WILAYANI KARATU



Na Mahmoud Ahmad,Karatu


Wazazi wa vijiji vya Kata ya  Barai iliyoko Wilayani Karatu Mkoani
Arusha wameiomba serikali ya awamu yaa tano  kuchunguza sababu za
watoto wao kufanya vibaya katika mitahani ya kuhitimu darasa la saba.



Wazazi hao wametoa kilio hicho kufuatia ufauulu  duni wa mara kwa mara
kwa watoto wanaohitimu darasa la saba ambapo wanafunzi hao wamekuwa
wanahitimu wakiwa hawajui kusoma wala kuandika na kushika nafasi za
mwisho kitaifa katika mtihani wa darasa la saba  jambo ambaalo
wanaliona  kama  kuwapotezea muda watoto hao ambapo wazazi hao  wakiwa
wanawaitaji kuwachungisha mifugo.




Aidha Kata hii  ya Barai yenye shule 12 za msingi ambapo kati ya shule
hizo shule  sita zimefanya vibaya kitaifa na zimeshikilia nafasi za
mwisho kabisa kitaifa ambapo alisema shule sita izo zipo katika nafasi
za shule kumi zilizofanya vibaya kitaifa katika mtiani wa darasa la
saba kwa mwaka jana.




Mwandishi wa habari hizi alitembelea    shule tatu za Kata hiyo  kujua
sababu zinazosababisha kutafaulu kabisa kwa wanafunzi  ambapo  taarifa
zinaonyesha kuwa   kuwa shuke hizo zina walimu sita pekee ikiwa na
maana kila shule yenye madarasa saba ina walimu wawili



Wakizungumzia sababu za shule hizo kufanya vibaya  mmoja wa mwalimu wa
shule ya msingi Gidamilanda Paul Hando alisema kuwa ni pamoja na
umbali mrefu ambao wanafunzi wanalazimika kutembea wakija mashuleni
ambapo wanatembea zaidi ya kilimeta 24 kwenda shuleni ,pamoja na
wanafunzi kutumia muda mwingi kuchunga mifugo badala ya kujisomea
pindi wanapotoka mashuleni.



Aidha alibainisha kuwa mbali na tatizo la umbali mrefu pia wanafunzi
wamkuwa wakisumbuliwa na tatizo la njaa kwani shule hizo zimekuwa
hasipikii wanafunzi mashuleni mchana kutokana  na kutokuwa na bajeti
hiyo .

Kwa upande wake mmoja wanafunzi hao ambao alijitambulisha kwa jina la
Gilony Gitonyi alisema kuwa wamekuwa wanashindwa kusoma kutokana na
njaa pamoja na kukosa mda wa kujisomea pindi wanaporudi nyumbani kwani
muda mwingi wamekuwa wakiutumia kwa ajili kuchunga mifugo pindi
wanaporudi majumbani.

Akizungumzia swala hilo  mbunge wa jimbo la karatu   Willy Qambalo
alisema kuwa kwa upande wake anaona  suluhisho la kutatua tatizo hilo
ni pamoja na  kujenga mabweni ilikuweza kuwasadia wanafunzi kupata
elimu ili kila mwanafunzi asome apoapo shuleni ili kuweza kujipatia
muda wa kujisomea.

"unajua  kujengwa kwa haya mabweni pia itasiadia kuwapata wanafunzi
kirahisi  ambao muda wamekuwa wakiacha masomo na kwenda kuchunga
mifugo jambo ambalo linapingwa vikali na wazazi wa vijiji hivyo na pia
wanafunzi hao watapata muda mrefu wa kujisomea na swala wao kupata
njaa litapungua kwani kutakuwa na chakula shuleni kwa ajili
yao"alisema Qambalo

Aidha Tafiti zinaonyesha walimu ,wenye utovu wa nidhamu watoro  na
walevi  katika maeneo ya mijini ndio hupelekwa katika shule hizzo
zilizoko maeneo ya porini kama adhabu kwao.Swali la kujiuliza je
mwalimu huyu atakuwa na nia ya kuwafundisha wanafunzi?Kupelekwa kwa
mwalimu huyu kama adhabu badala ya eyey kuridhia  Kujua kusomaa na

kandika kwa wanafunzi hawa itakuwa ni ndoto

WAJASIRIAMALI WAKULIMA NA WAFUGAJI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO YA MASHINE BILA DHAMANA

ab3c2a4b-b9c3-4f15-8bf3-ab71acab0bf7
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
………………………………………………………………………………………………….
Mahmoud Ahmad Arusha
Wajasiriamali kote nchini wakiwamo pia wakulima na wafugaji nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya mikopo ya vifaa ikiwemo trekta na mashine mbali mbali za kilimo na ufugaji sambamba na
vifaa mbali mbali lengo likiwa ni kukuza kipato kwa wananchi.
Akizungumza na waanahabari meneja mikopo wa kampuni ya Wasambazaji wa vifaa kutoa mikopo kwa wajasiriamali bila dhamana yeyote (EFTA)yenye makao makuu yake Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Peter Temu amesema kuwa wanawakaribisha wananchi kwenye maonyesho hayo ya siku tatu yakatayofanyika mkoani hapa.
Amesema kuwa kwenye maonyesho hayo zaidi ya wauzaji na wasambazaji wa mashine 25 watakuwa wakionyesha bihdaa na mashine walizonazo kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wananchi watakaoudhuria ili wajue matumizi bora ya mashine aina,mashine halisi,waranti na mabo mengine mbali mbali bila ya kiingilio.
Alisema kuwa mbali na maonyesho hayo ya EFTA pia wamejianda kuwafanya watembeleaji wa mabanda ya maonyesho hayo kuona na kupata mambo mengi ya ziada ikiwemo kupata semina na mafunzo kwa wajasiriamali toka kwa wataalamu mbali mbali bila malipo.
“Mafunzo haya yatatolewa bure na wataalamu wenye uzoefu na masuala ya ujasiriamali na kilimo ili wakulima na wajasiriamali wapate faida ya shughili wanazofanya kama kuongeza thamani katika bidhaa wanazozalisha na vifungashio vya kilimo na viwandani”alisema Temu
Alisema hiyo itakuwa fursa muhimu nay a kipekee kwa watanzania watakaobahatika kufika kwenye viwanja vya makumbusho kwa siku tatu kuanzia Alhamisi hadi yatakapofungwa jumamosi huku wakitarajia wakazi wengi kutoka mikoa ya kaskazini ikiwemo Kilimanjaro,Tanga,Arusha na Manyara kuchangamkia na kufika kukutana na wauzaji na was am,bazaji hawa huku wakijua kuwa EFTA LTD inafanya nn kwa ajili yao katika shughuli nzima ya utoaji wa mikopo bila dhamana na kutoa huduma ya mikopo  moja kwa moja kwa wajasiriamali na wakulima wote watakaofika katika maonyesho hayo.
“Tunaposema mashine za kila Aina tunamaanisha anazohitaji mteja na sio kuwa tunamchagulia mteja,mfano mashine na vifaa vya kilimo,mashine za kufyatulia matofali,mashine za kukamulia alizeti vifaa vya maabara mashine za kutengeneza chakula cha mifugo na kutotolea vifaranga pamoja kilimo cha umwagiliaji na green house na nyingine nyingi’’Alisema Temu

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA AFUNGA MACHIMBO YA MORAMU MOSHONO



picha kwa hisani ya  maktaba

Na Mahmoud Ahmad,Arusha

Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkurlu amesimamisha shughuli za uchimbaji katika machimbo ya moramu katika kata ya Moshono Mkoani Arusha kwa kipindi cha mwezi mmoja kupisha wakandarasi kuweka sawa machimbo hayo ambayo yanachimbwa bila kufuata utaalamu hali ambayo inadaiwa inaweza kuhatarisha uhai wa maisha yao.


Katika kipindi cha mwaka 2013 machimbo hayo yaliuwa wachimbaji 13 hali ambayo ilimfanya waziri mkuu mstaafu Peter Pinda kuyafunga mpaka yatakaporekebishwa ndiyo wachimbaji hao waendelee na uchimbaji ingawa inadaiwa wachimbaji hao hawakufuata maagizo mpaka hivi sasa kwani waliendelea na shughuli za uchimbaji.

Akizungumza wakati akifunga machimbo hayo mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhil Nkurlu alisema kuwa mazingira ya wachimbaji hao ni mabaya na yanahatarisha maisha yao kwa kiasi kikubwa na kwamba hawana utaalamu wa kutosha juu ya namna bora ya uchimbaji wa moramu hiyo mbali na kuchimba kinyemela toka kauli ya waziri mkuu kutamkwa.

Alisema kuwa ameamua kufunga machimbo hayo kutokana na oanagezeko kubwa la vifo linalosabibishwa na uchimbaji wa moramu usiozingatia sheria na kanuni .


 Naye kamishina msaidizi wa madini kanda ya kaskazini Elias Kadabila alichukuwa fursa hiyo kuwaomba wananchi kufuata maelezo ya mkuu wa wilaya  ili waweze kuchimba kuchimba kwa usala  ambapo alisema kuwa pia iatawasaidia  kuepukana na maafa au vifo vinavyotokana na uchimbaji holela.

Aidha pia aliuomba uongozi wa mtaa pamoja na wachimbaji hao kutoa ushirikiano ili kuweza kuwapisha wakandarasi kutengeneza machimbo hayo kwa muda wa mwezi mmoja .

Gazeti hili pia liliweza kuzungumza na baadhi ya wachimbaji hao  ambapo walisema kuwa hawakubaliani na agizo hilo la mkuu huyo kwakuwa uchimbaji huo ndiyo ambao unawafanya kumudu gharama za maisha na kusomesha watoto na kwamba serikali iangalie namna nyingine.

"kwakweli tunaomba serekali iangalie tena na tena swala hili kwani sisi wananachi ndio tunategemea maachimbo haya kwani ndio yanatusaidia tunaweza kula ,kusomesha watoto ,kujenga naweza sema kiujumla kuendesha maisha yetu"Alisema Lowayani Metili


 Ipo haja ya wachimbaji hao kupisha marekebisho hayo yatakayofanywa na serikali kwa manufaa yao na uhai wao kwani kuendelea kuchimba wakati wanahatarisha maisha yao ni jambo la hatari Zaidi kwani wahenga wanamsemo usemao UHAI NI BORA KULIKO KIFO.

PROF. MBARAWA ATOA MWEZI MMOJA KWA MAKANDARASI.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo kuhusu ukusanyaji madeni ambayo Wakala wa Majengo nchini (TBA) inadai wapangaji wake. 
 Muonekano wa barabara ya Sakina-Tengeru Km 14.1 inayojengwa kwa njia nne kwa kiwango cha lami ili kupunguza msongamano wa magari kuingia na kutoka katikati ya jiji la Arusha. 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Fadhili Nkurlu jijini Arusha.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia) akikagua ripoti ya biashara inayofanywa na Kampuni ya Simu nchini (TTCL), jijini Arusha. Wa tatu kulia ni Meneja Kanda ya Kaskazini TTCL Bw. Peter Lusama. 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) akiimba wimbo wa mshikamano daima na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS kabla ya kufungua rasmi mkutano wa sita wa Baraza hilo. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale na kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Fadhili Nkurlu. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza kufanya kazi kwa malengo yanayopimika katika kikao chake na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya wizara yake, jijini Arusha. 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mkandarasi M/S Hanil Jiangsu J/V anayejenga barabara ya Sakina-Tengeru Km 14.1 na barabara ya mchepuo wa kusini Arusha bypass Km 42.4 jijini Arusha.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. 


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametoa mwezi mmoja kwa makandarasi wote nchini kuhakikisha wanasaini mikataba ya ajira na wafanyakazi katika miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea nchini kote.
Akizungumza jijini Arusha mara baada ya kufanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa Km 14.1 na barabara ya mchepuo ya kusini (Arusha bypass) yenye urefu wa Km 42.4, Prof. Mbarawa amesema mkandarasi atakayeshindwa kutoa mikataba kwa mujibu wa sheria za Tanzania, atanyang’anywa kazi ya ujenzi kwa kuvunja sheria.
“Barabara zinajengwa kwa kodi za wananchi hivyo wajenzi wa barabara nao ni lazima wafuate sheria za nchi ili kuhakikisha Serikali inapata kodi stahili na wafanyakazi wazawa nao wanapata haki stahili kwa mujibu wa ajira zao", amesema Waziri Prof. Mbarawa. 
Amezitaka taasisi za TRA, NSSF na nyingine zinazosimamia ajira za wafanyakazi kufuatilia miradi ya ujenzi ili kuona fursa za mapato ambazo serikali inaweza kupata na kusajili wafanyakazi katika hifadhi ya mifuko ya jamii.
Waziri Prof. Mbarawa amewataka mameneja wa tanroads na maafisa kazi kukagua mikataba ya ajira za ujenzi katika maeneo yao ili kuona haki inatendeka kwa makandarasi na kwa wafanyakazi ili ujenzi wa barabara ukamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amefungua mkutano wa Sita wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na kuwataka kuweka mikakati itakayowezesha kulinda hifadhi ya barabara, kudhibiti magari yanayozidisha uzito na kusimamia kasi katika miradi ya ujenzi wa barabara.
“Mmekua mkifanya kazi nzuri, endeleeni kufanya kazi kwa uadilifu, uwazi, weledi na kujiwekea malengo ya kujipima mwaka hadi mwaka ili muendelee kuwa tassisi ambayo watu watakuja kujifunza kwenu”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Naye Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa TANROADS imejipanga kuhakikisha miradi ipatayo 90 ya ujenzi wa barabara inayoendelea nchini kote inakamilika katika ubora unaotakiwa na unao uwiana na thamani ya fedha.
Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amemuagiza Meneja wa Wakala wa Majengo nchini (TBA), mkoa wa Arusha, Bw. Victor Baltazar kukusanya madeni yote kwa haraka ili kukamilisha miradi ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na za biashara inayosimamiwa na Wakala huo mjini Arusha kukamilika kwa wakati.
Prof. Mbarawa ambaye yuko katika ziara ya mikoa ya kanda ya kaskazini amezitaka taasisi zilizo chini wa wizara hiyo kuhakikisha zinafanya kazi kibiashara ili kuboresha mapato ya Serikali na hivyo kuiwezesha Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

ELIMU BORA ITOKANE NA WALIMU BORA – MELISA

Kushoto ni Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akikabidhi tuzo za Walimu Bora kwa mshindi wa Kwanza Maganga Lorry wa shule ya msingi Mbaaseny ,katikati ni Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tomorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akizungumza katika utoaji wa tuzo za Walimu Bora ,,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.Picha na Ferdinand Shayo
Kushoto ni Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akikabidhi tuzo za Walimu Bora kwa mshindi wa 5 Mwalimu Clara Ernest wa shule ya Msingi Tuvaila , katikati ni Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tomorrow (TFFT)N,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo naMzawadi mbalimbali.
washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
Washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.

Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akizungumza na walimu katika Halfa ya Utoaji tuzo za walimu bora kwa walimu wa shule za msingi wilaya ya Meru zilizofanyika jana ,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
Washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.Picha na Ferdinand Shayo

                                             Na Mahmoud Ahmad ,Arusha.

Serikali imetakiwa kuboresha mazingira bora ya walimu ili kukuza na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani walimu ni kiungo muhimu katika elimu ambacho kinapaswa kupewa kipaumbele kwenye kutimiza azma ya serikali kutoa elimu bora kwa Watanzania.


Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tomorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen ameyasema hayo jana wakati wa utoaji wa tuzo za walimu bora wa shule za msingi za serikali kwa kutambua mchango wa walimu katika maendeleo ya elimu nchini na ustawi bora wa jamii .

Melisa alisema kuwa maendeleo ya taifa lolote lile yanategemea ubora wa elimu waliyonayo watu wake hivyo ni vyema serikali inapofikiria kuboresha elimu ifikirie kuboresha mazingira ya walimu kuanzia kitaaluma wanapoandaliwa kwenda kufundisha ,vifaa vya kufindishia pamoja na stahiki zao.

“Bila Walimu Bora hakuna Elimu Bora ,Tumeamua kuwatia moyo wa walimu kwa kutoa tuzo hizi na vyeti vya kutambua mchango wao ,washindi ni 10 mshindi wa kwanza amepatiwa cheti na shilingi la kitano,na washindi wengine tumewapatia vyeti na fedha taslimu” Alisema Melisa

Afisa Elimu wa Shule za Msingi Wilaya ya Meru Tumsifu Mushi amewataka walimu kufanya kazi ya ualimu kwa moyo na kwa kujituma huku wakitambua kuwa wana wajibu mkubwa wa kuandaa wataalamu watakaoisaidia jamii,taifa
na duni jukumu ambalo ni nyeti linapaswa kubebwa kwa uzito unaostahili.

Kwa upande wao walimu waliopewa tuzo hizo Rose Salim wa shule ya Msingi Uraki na Ekaeli Newasha wa Shule ya msingi Kimundo wamesema kuwa kundi la walimu limekua likisahaulika mchango wake katika jamii hivyo tuzo hizo Zimeamsha ari na hamasa ya kufanya kazi kwa bidii.

“Kazi ya ualimu unapaswa uwe unapenda watoto unapenda kuwasaidia waweze kufika mbali kitaaluma ,binafsi nimefanya kazi hii kwa miaka mingi na ninaipenda sana” Alisema Mwalimu Rose Salim