Na Mahmoud Ahmad,Karatu
Wazazi wa vijiji vya Kata ya Barai iliyoko Wilayani Karatu Mkoani
Arusha wameiomba serikali ya awamu yaa tano kuchunguza sababu za
watoto wao kufanya vibaya katika mitahani ya kuhitimu darasa la saba.
Wazazi hao wametoa kilio hicho kufuatia ufauulu duni wa mara kwa mara
kwa watoto wanaohitimu darasa la saba ambapo wanafunzi hao wamekuwa
wanahitimu wakiwa hawajui kusoma wala kuandika na kushika nafasi za
mwisho kitaifa katika mtihani wa darasa la saba jambo ambaalo
wanaliona kama kuwapotezea muda watoto hao ambapo wazazi hao wakiwa
wanawaitaji kuwachungisha mifugo.
Aidha Kata hii ya Barai yenye shule 12 za msingi ambapo kati ya shule
hizo shule sita zimefanya vibaya kitaifa na zimeshikilia nafasi za
mwisho kabisa kitaifa ambapo alisema shule sita izo zipo katika nafasi
za shule kumi zilizofanya vibaya kitaifa katika mtiani wa darasa la
saba kwa mwaka jana.
Mwandishi wa habari hizi alitembelea shule tatu za Kata hiyo kujua
sababu zinazosababisha kutafaulu kabisa kwa wanafunzi ambapo taarifa
zinaonyesha kuwa kuwa shuke hizo zina walimu sita pekee ikiwa na
maana kila shule yenye madarasa saba ina walimu wawili
Wakizungumzia sababu za shule hizo kufanya vibaya mmoja wa mwalimu wa
shule ya msingi Gidamilanda Paul Hando alisema kuwa ni pamoja na
umbali mrefu ambao wanafunzi wanalazimika kutembea wakija mashuleni
ambapo wanatembea zaidi ya kilimeta 24 kwenda shuleni ,pamoja na
wanafunzi kutumia muda mwingi kuchunga mifugo badala ya kujisomea
pindi wanapotoka mashuleni.
Aidha alibainisha kuwa mbali na tatizo la umbali mrefu pia wanafunzi
wamkuwa wakisumbuliwa na tatizo la njaa kwani shule hizo zimekuwa
hasipikii wanafunzi mashuleni mchana kutokana na kutokuwa na bajeti
hiyo .
Kwa upande wake mmoja wanafunzi hao ambao alijitambulisha kwa jina la
Gilony Gitonyi alisema kuwa wamekuwa wanashindwa kusoma kutokana na
njaa pamoja na kukosa mda wa kujisomea pindi wanaporudi nyumbani kwani
muda mwingi wamekuwa wakiutumia kwa ajili kuchunga mifugo pindi
wanaporudi majumbani.
Akizungumzia swala hilo mbunge wa jimbo la karatu Willy Qambalo
alisema kuwa kwa upande wake anaona suluhisho la kutatua tatizo hilo
ni pamoja na kujenga mabweni ilikuweza kuwasadia wanafunzi kupata
elimu ili kila mwanafunzi asome apoapo shuleni ili kuweza kujipatia
muda wa kujisomea.
"unajua kujengwa kwa haya mabweni pia itasiadia kuwapata wanafunzi
kirahisi ambao muda wamekuwa wakiacha masomo na kwenda kuchunga
mifugo jambo ambalo linapingwa vikali na wazazi wa vijiji hivyo na pia
wanafunzi hao watapata muda mrefu wa kujisomea na swala wao kupata
njaa litapungua kwani kutakuwa na chakula shuleni kwa ajili
yao"alisema Qambalo
Aidha Tafiti zinaonyesha walimu ,wenye utovu wa nidhamu watoro na
walevi katika maeneo ya mijini ndio hupelekwa katika shule hizzo
zilizoko maeneo ya porini kama adhabu kwao.Swali la kujiuliza je
mwalimu huyu atakuwa na nia ya kuwafundisha wanafunzi?Kupelekwa kwa
mwalimu huyu kama adhabu badala ya eyey kuridhia Kujua kusomaa na
kandika kwa wanafunzi hawa itakuwa ni ndoto
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni