KOCHA STEVE McCLAREN ATIMULIWA KAZI NEWCASTLE UNITED

Timu ya Ligi Kuu ya Uingereza ya Newcastle United imemtimua kazi kocha wake mkuu Steve McClaren.

Kocha huyo wa zamani wa Uingereza ameshinda mechi sita tu kati ya 28 za Ligi Kuu ya Uingereza akiinoa Newastle ambayo ni ya pili kutoka mkiani.

Kocha McClaren na timu yake walizomewa kufuatia kipigo cha jumamosi cha mabao 3-1 kutoka kwa Bournemouth katika dimba la St James' Park.

Kocha wa zamani wa Liverpool, Chelsea, Real Madrid na Inter Milan, Rafael Benitez anawaniwa kuchukua nafasi yake.
                          Rafa Banitez akichekelea uwezekano wa kupata kibarua hicho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni