Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Mhe. Said Meck Sadiki kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Dkt. Rehema Nchimbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Mhe. Said Thabit Mwambungu  kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Mhe. Magesa Mulongo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara katika hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Mhe. Amina Juma Masenza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa leo Ikulu jijini Dar es salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Mhe. Halima Omary Dendegu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Mhe. Jordan Mungire Rugimbana kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven  kuwa  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Mhe. Paul Makonda  kuwa  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Ikulu jijini Dar es salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga kuwa  Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga  kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Valentino Mlowola aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Alphayo Kidata kuwa  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
 Baadhi
 ya Wakuu wa Mikoa wakiimba wimbo wa Taifa kabala ya kuapishwa na Rais 
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Wakuu wa Mikoa wapya wa Tanzania Bara walioapishwa leo wakiwa katika picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es salaam.
 Wakuu
 wa Mikoa wapya walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 
Dkt. John Pombe Magufuli wakila kiapo cha kuzingatia maadili ya viongozi
 wa umma katika kutekeleza majukumu yao leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Wakuu
 wa Mikoa wapya walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 
Dkt. John Pombe Magufuli wakisaini hati za viapo vya maadili ya viongozi
 wa umma mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es 
salaam.Picha/Eleuteri Mangi na Aron Msigwa.
Na Jacquiline Mrisho- Dar es salaam.     
Rais
 wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli 
amewapa siku 15 Wakuu wa Mikoa kuwaondoa watumishi hewa walio katika 
orodha ya malipo ya mishahara ya watumishi wa umma katika Mikoa yao.
Rais
 Dkt. Magufuli amesema hayo leo Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya 
kuwaapisha Wakuu wa Mikoa aliowateua Machi 13 mwaka huu ambapo 
amewaagiza washirikiane na Wakurugenzi wa Halmashauri kuwaondoa 
watumishi hewa.
“Nimewapa
 siku 15 kuanzia leo mkashirikiane na Wakurugenzi wa Halmashauri zenu 
kuwatoa wafanyakazi hewa, nikigundua kuwa bado kuna wafanyakazi hewa, 
Mkurugenzi husika atafukuzwa kazi na atapelekwa mahakamani”,
Na
 kusisitiza “Nimeamua kuwachagua nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri 
katika Mikoa yenu, nawaomba mkatimize majukumu yenu bila kuogopa” 
alisema Dkt. Magufuli.
Aidha,
 Mhe.  Dkt. Magufuli amesikitishwa na utafiti wa watumishi uliofanywa 
katika Mikoa ya Singida na Dodoma ambapo imegundulika watumishi 202 
wanalipwa mishahara hewa.
Wakati
 wa utafiti huo, zaidi  ya watumishi 26,900 walioko katika Halmashauri 
14 za Mikoa hiyo, watumishi 3,320 hawakuwepo kazini kwa sababu 
mbalimbali.
Kwa
 mantiki hiyo, ukichukua utafiti huo wa Mikoa miwili ni dhahiri Serikali
 inapoteza mapato mengi kwa kulipa mishahara ya watumishi hewa nchi 
nzima.
Vivyo
 hivyo, Mhe. Dkt. Magufuli amewasisitiza Wakuu wote wa Mikoa wakasimamie
 ilani ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwakuwa waliahidi 
kutatua kero za wananchi na wahakikishe wanazitatua ili wananchi waishi 
vizuri kwa amani ndani ya nchi yao.
Naye
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa Mikoa na 
Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri zote nchini wajiandae kupokea na 
kuzipangia matumizi shilingi milioni 50 za kila Kijiji zilizoahidiwa 
wakati wa kampeni kwa lengo 
la kuboresha na kuimarisha shughuli za 
maendeleo.
Wakuu Wateule wa Mikoa wakisubiri kuapishwa na Rais 
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo naMh Angellah Kairuki
Wakuu wa Mikoa wapya kabla ya kuapishwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri Ikulu,mapema leo jijini Dar
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo viongozi wa Ulinzi na Usalama 
Wakuu wa Mikoa wakitia Saini hati kiapo cha Maadili ya viongozi wa  Umma leo mara baada kuapishwa Ikulu jijini Dar


















Hakuna maoni:
Chapisha Maoni