Kamishna
Jenerali wa Magereza John C. Minja( wa pili kushoto) akikagua maeneo
mbalimbali ya Gereza Bukoba alipofanya ziara ya kikazi leo Machi 11,
2016 (wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera, SACP. Omari
Mtiga (wa pili kulia) ni Mkuu wa Gereza Bukoba, ACP. Benizeth Bisibe.
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella akiongea ofisini kwake na Kamishna
Jenerali wa Magereza John C. Minja na ujumbe wake (hawapo pichani)
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella akiongea ofisini kwake na Kamishna
Jenerali wa Magereza John C. Minja na ujumbe wake kama inavyoonekana
katika picha.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba Mhe. Sivangilwa Mwangesi
Akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza John C. Minja
alipomtembelea ofisini kwake.
Kamishna
Jenerali wa Magereza John C. Minja (wa nne kushoto) akiwa katika picha
ya pamoja na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoani Kagera mara
baada ya kutembelea Gereza la Wilaya ya Bukoba (Picha na Lucas Mboje wa
Jeshi la Magereza).
Kamishina Jenerali wa
Mageraza nchini John Carmir Minja afanya ziara ya kikazi Mkoani Kagera
yenye lengo la kutembelea na kukagua Magereza ya Mkoa wa Kagera pamoja
na kujionea miradi ya uzalishaji inayosimamiwa na Jeshi hilo.
Akiwa
Mkoani hapa Kamishna Jenerali Minja alifika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa
Kagera Mhe. John Mongella na kufanya naye mazungumzo kuhusu utendaji
kazi na ufanisi wa Jeshi la Magereza Mkoani hapa katika kuimarisha
ulinzi na usalama.
Aidha katika mazungumzo hayo walizungumzia
changamoto ya msongamano wa Mahabusu katika Gereza la Wilaya ya Muleba
ambalo hivi sasa linatumika kuhifadhi Mahabusu wa Wilaya ya Muleba na
Wilaya ya Chato Mkoani Geita ambayo haina Gereza la Wilaya.
Kamishna
Jenerali wa Mageraza nchini John Carmir Minja pia alitembelea Mahakama
Kuu Kanda ya Bukoba na kufanya mazungumzo na Jaji Mfawidhi wa Mahakama
hiyo Mhe. Sivangilwa Mwangesi juu ya namna ya kuongeza kasi ya
usikilizwaji wa kesi mbalimbali za watuhumiwa ili kuondoa msongamano
Magerezani.
Vilevile Kamishna Jenerali Minja alitembelea Gereza
la Wilaya la Bukoba na kuongea na wafungwa na Mahabusu wa Gereza hilo
pia na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la zahanati ambalo lipo katika
hatua za mwisho kukamilishwa ili liweze kutoa huduma za afya kwa
wafungwa na watumishi wa Jeshi hilo pamoja na wananchi wanaoishi jirani
na zahanati hiyo.
Kamishna Jenerali Minja yupo Mkoani Kagera kwa
siku 7 kuanzia tarehe 10 hadi 16 Machi, 2016 ambapo lengo la ziara hiyo
ni kutembelea na kukagua Magereza ya Mkoa wa Kagera pamoja na kujionea
miradi ya uzalishaji inayosimamiwa na jeshi hilo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni