ABIRIA AEPUSHA AJALI BAADA YA KUONA SPANA KWENYE BAWA LA NDEGE

Ndege ya EasyJet iliyokuwa ikitokea Geneva imelazimika kusita kuruka dakika chache kabla ya kuanza kuondoka baada ya mmoja wa abiria kuona spana kwenye bawa la ndege.

Ndege hiyo ya abiria ilishakuwa imeruhusiwa kuanza kuelekea kwenye njia ya kupaa, ndipo abiria mmoja raia wa Uswizi alipoona spana na kuwaarifu wahudumu wa ndege.

Rubani wa ndege ilibidi airejeshe ndege katika eneo la maegesho na spana hiyo kuondolewa, ambapo uchunguzi umeanza kufanywa juu ya tukio hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni