SERIKALI YA SUDAN KUSINI LAWAMANI KWA KUUWA WATU 60 KIKATILI

Shirika la kutetea haki za binadamu limesema linaushahidi kuwa vikosi vya serikali ya Sudan Kusini, viliwauwa wanaume 60 wakiwemo wavulana kwa kuwafungia ndani ya kontena na kukosa hewa.

Baada ya kufanya hivyo vikosi hivyo vya serikali viliitupa miili ya watu hao kwenye mji wa Leer katika jimbo la Unity, shirika la Amnesty International limesema.

Maelfu ya watu wameuwawa Sudan Kusini na mamilioni wameachwa bila ya makazi tangu mwaka 2013.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni