BONDIA MANNY PACQUIAO AWASILI JIJINI LOS ANGELES KUJIANDAA NA PAMBANO

Bondia Manny Pacquiao amewasili Jijini Los Angeles tayari kwa kukamilisha pambano lake la mwisho kabla ya kustaafu.

Bondia huyo ametua katika uwanja wa ndege wa LAX, na kulakiwa na mashabiki wake pamoja na vyombo vya habari kabla ya kuingia kambini.

Pacquiao atapambana na Timothy Bradley Jr kwa mara ya tatu Aprili 9, ikiwa karibia mwaka mmoja kupita tangu pambano lake la mwisho. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni