Muwania urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican, Marco Rubio
amemshambulia mwenzake Donald Trump kwa kusema kuwa Uislam unaichukia
Marekani, katika mdahalo uliorushwa kwenye televisheni huko Miami.
Bw. Rubio, ambaye anakazi kubwa ya kupambana hadi kufa kushinda
kura za maoni za wanachama huko Florida jumanne, amesema kuna tatizo
la itikadi kali katika Uislam, lakini waislamu wengi wanajivunia
Marekani.
Mgombea huyo amemkubusha Bw. Trump kwamba marais hawapaswi
kusema kila wanachotaka kusema, kwani kwa kufanya hivyo kunaweza
kusababisha madhara, kauli ambayo ilishangiliwa mno na watu
waliohudhuria mdahalo huo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni