Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Dk. Juliana Pallangyo
(pichani) akifungua mkutano unaoshirikisha wakurugenzi wa mashirika ya umeme
katika nchi zilizopo kusini mwa Afrika zinazoshirikiana katika biashara ya
umeme.
Sehemu
ya watendaji na wakurugenzi wa mashirika ya umeme katika nchi zilizopo kusini
mwa Afrika zinazoshirikiana katika biashara ya umeme, wakifuatilia hotuba
iliyokuwa inatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia masuala ya nishati, Dk.
Juliana Pallangyo (hayupo pichani).
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati, Dk. Juliana Pallangyo
(kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Mhandisi Decklan
Mhaiki (kushoto) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na mwenyekiti wa
kamati ya nchi za kusini mwa Afrika zinazoshirikiana katika biashara ya umeme, Josh Chifamba (hayupo pichani)
Mwenyekiti
wa kamati ya nchi za kusini mwa Afrika zinazoshirikiana katika biashara ya
umeme, Josh Chifamba (kulia) akimkabidhi zawadi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia
masuala ya nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) aliyekuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mkutano huo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati, Dk. Juliana Pallangyo
(aliyekaa mbele katikati) akiwa katika
picha ya
pamoja na sehemu ya watendaji na
wakurugenzi wa mashirika ya umeme katika nchi zilizopo kusini mwa Afrika
zinazoshirikiana katika biashara ya umeme, mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
Na
Greyson Mwase, Dar es Salaam
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati,
Dk Jualiana Pallangyo amewataka
wawekezaji binafsi nchini kujitokeza kwa wingi na kuwekeza katika uzalishaji na
uuzaji wa nishati ya umeme nchini
ili iweze kuchangia katika ukuaji wa
uchumi wa nchi.
Dk.
Pallangyo alisema hayo kwenye mkutano unaokutanisha wakurugenzi wa mashirika ya
umeme katika nchi zilizopo kusini mwa Afrika zinazoshirikiana katika biashara
ya umeme. Nchi hizo ni pamoja na
Bostwana, Msumbiji, Afrika ya Kusini, Lesotho, Namibia, Jamhuri ya
Demokrasia ya Kongo, Swaziland, Zambia na Zimbabwe. Lengo la mkutano huo wa
siku moja lilikuwa ni kujadili changamoto zinazozikumba nchi wanachama katika
uzalishaji na uuzaji wa umeme ikiwa ni pamoja na kubadilishana
uzoefu.
Aliongeza
kuwa wawekezaji binafsi wanaweza
kuzalisha umeme kupitia vyanzo mbalimbali vya nishati ikiwa ni pamoja
na maporomoko madogo ya maji, upepo, bayomasi na jua kutokana na uwezo wao.
Akielezea
fursa za uwekezaji nchini, Dk. Pallangyo alisema kuwa wawekezaji wanaweza
kuwekeza kupitia ujenzi wa miundombinu
ya usambazaji wa umeme, uendelezaji wa
miradi ya umeme unaotokana na maporomoko madogo ya maji na vyanzo
vingine ikiwa ni pamoja na
jotoardhi, upepo na uanzishwaji wa viwanda vidogo kwa ajili ya utengenezaji wa
vifaa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya umeme.
Dk.
Pallangyo aliongeza kuwa ushiriki wa
sekta binafsi katika sekta ya
umeme umeongezeka kila mwaka na kusisitiza kuwa serikali bado inaendelea na
mikakati ya kuwawezesha wawekezaji binafsi
katika uzalishaji ya umeme
nchini.
Aliongeza
kuwa serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini ikiwa ni pamoja na sera na sheria
mbalimbali zinazotumika kama mwongozo na
kutaja kuwa ni pamoja na sheria ya umeme ya mwaka 2008, sera ya nishati ya mwaka 2003 ambayo
inahamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika sekta ya umeme.
Alitaja
sheria nyingine kuwa ni pamoja na ile ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ya mwaka
2001, sheria ya Wakala wa Nishaji Vijijini (REA) ya mwaka 2005.
Akielezea
mikakati ya serikali katika upatikanaji wa nishati ya uhakika, Dk. Pallangyo alisema kuwa serikali
imeweka mkakati wa kuhakikisha kuwa
ifikapo mwaka 2025 asilimia 75 ya wananchi wote hasa waishio vijijini wanapata nishati ya umeme ambayo ni
ya uhakika.
“Tunatarajia
kuzalisha hadi megawati 10,000 za umeme
ambao utachochea ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia viwanda na hivyo nchi kutoka
katika kundi la nchi masikini duniani na kuwa
katika kundi la nchi zenye kipato cha kati duniani,” alisisitiza Dk. Pallangyo.
Akielezea
hali ya upatikanaji wa umeme nchini, Dk. Pallangyo alisema kuwa umeme
unaozalishwa ni megawati 1461.69 huku mahitaji halisi yakiwa ni megawati 1026.
Umoja
wa nchi zinazoshirikiana katika sekta ya
umeme kusini mwa Afrika (Southern African Power Pool; SAPP) ulianzishwa Agosti
mwaka 1995 katika Mkutano wa Umoja wa
Nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara
(SADC) ambapo walisaini makubaliano kwa ajili ya kushirikiana katika uzalishaji na biashara
ya umeme wa pamoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni