WAHAMIAJI WATUMIA NJIA HATARI YA KUKATIZA MTONI KUINGIA ULAYA

Mamia ya wahamiaji waliokwama katika kambi Ugiriki wanahatarisha maisha yao kwa kukatiza mto wenye maji katika kujaribu kuingia Ulaya.

Njia hiyo hatari tayari imechukua maisha ya wakimbizi watatu akiwemo mwanamke mjamzito ambaye mwili wake umeibuliwa kutoka majini karibu na mpaka wa Macedonia hii leo.

Lakini saa chache baadaye wahamiaji wengine wapatao 1,000 wakiwemo wanawake, watoto na hata mtu mlemavu aliye kwenye kiti cha magurudumu walikuwa wakijaribu kukatiza mto huo baada ya kuelezwa hakuna uzio katika upande wa pili.
           Mwanamke akisaidiwa kuvuka kwenye mtu huo na wahamiaji wenzake
Ni safari hatari lakini yenye matumaini ya kuingia Ulaya na kupata maisha bora kwa wahamiaji hawa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni