Wafanyakazi wanawake wa TBL Group wa Mwanza,Mbeya na Arusha wapatiwa elimu ya mafanikio


 Bi.Anne Killango Malecela akitoa somo
 Wanawake wa TBL Arusha katika picha ya pamoja na Bi.Killango
 Wanawake wa TBL Mbeya wakipata burudani na Mkuu wa wilaya
 Jaji De-Mello akiongea na wanawake wa TBL Group wa Mwanza
 
 Mkuu wa wilaya ya Kyela Bi.Ntara akitoa somo
Baadhi ya washiriki wa TBL forum Mwanza wakiwa  kwenye picha ya pamoja
Baadhi ya washiriki wa Forum wa  Arusha wakiwa na   Bi.Killango 
Wafanyakazi  wanawake wa TBL Group wa  Mwanza,Mbeya na Arusha  wapatiwa elimu ya mafanikio
-Ni kupitia makongamano ya TBL Forum
Kampuni ya TBL Group mwishoni mwa wiki iliandaa kongamano la kuwajengea uwezo wa mbinu za mafanikio kwa wafanyaazi wanawake katika mikoa ya Arusha,Mbeya na Mwanza ambapowalipata kujifunza mbinu za mafanikio na jinsi ya kujiamini katika  kazi zao.
Wazungumzaji wakuu katika kongamano hilo  la TBL Women Forum walikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kyela,Bi.Thea Ntara (Mbeya),Bi.Anne Malecela Killango (Arusha) na Jaji Joaquine De-Mello ambao walitumia elimu na uzoefu mkubwa walionao katika kazi kuwaelimisha waawae wenzao mbinu za kupata mafanikio ambapo walisisitiza kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi na kujiamini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni