Modest Apolinary Meneja na Kaimu
Mkurugenzi wa mgodi wa Tanzanite One akiwaomyesha wahariri mbalimbali wa
vyombo vya habari mipaka ya mgodi huo, wakati wahariri hao
walipoutembelea mgodi wa huo uliopo Mererani wilayani Simanjiro katika
mkoa wa manyara kwa ajili ya kuangalia na kujifunza kuhusu shughuli
mbalimbali zinazoendeshwa katika mgodi huo ambao kwa sasa unamilikiwa na
kampuni ya watanzania inayoitwa Sky Asocciate.
Mgodi huo unaendeshwa kwa ubia
pamoja na shirika la madini la STAMICO, Bw. Modest Apolinary
amelalamikia kampuni ya Bw.Said Nasoro maarufu kama (Mwarabu) kwa
kuingia kwenye eneo la Tanzanite One la Kitalu C chinimkwa chini na
kukutana na njia za mgodi wa kampuni ya Tanzanite One maarufu kama
(mtobozano) jambo ambalo limeifanya kampuni ya Tanzanite One kufunga
baadhi ya migodi yake kwa sababu za kiusalama na uchimbaji usio na
tija. (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MERERANI MANYARA)
Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakielekea Mererani kwa ajili ya kutembelea mgodi wa Tanzanite One mkoani Manyara leo.
Wahariri wa vyombo mbalimbali vya
habari wakitembelea na kujionea baadhi ya migodi ya Tanzanite One
katika Kitalu C iliyofungwa kutokana na kuingiliwa na wachimbaji wadogo.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri
TEF Mzee Theophil Mkubga akiongoza wahariri wenzake ili kujionea mipaka
ya kampuni ya Tanzanite One iliyoingiliwa na wachimbaji wadogo.
Mkuu wa Usalama wa kampuni ya Tanzanite One Bw. George Kisambe akiwaonyesha wahariri mipaka ya mgodi huo.
Mkuu wa Usalama wa kampuni ya
Tanzanite One Bw. George Kisambe akiwaeleza jambo wakati akiwaonyesha
wahariri mipaka ya mgodi huo.
Modest Apolinary Meneja na Kaimu
Mkurugenzi wa mgodo wa Tanzanite One akiwaomyesha wahariri wa vyombo vya
habari mipaka ya mgodi huku kwa mbali ukionekana mgodi uliofungwa
mbele yao mgodi huu upo kitalu C na unapakana na Kitalu D cha
wachimbaji wadogo.
Modest Apolinary Meneja na Kaimu
Mkurugenzi wa mgodo wa Tanzanite One akiongozana na wahariri wa vyombo
vya habari mara baada ya kujionea mipaka ya mgodi
Mhariri wa Jambo leo Bw. Joseph
Kulangwa akisalimiana na Mwanafunzi wake mhandisi Kimonge Kiravo wakati
wahariri walipotembelea katika mgodi wa Tanzanite One leo.
Mhandisi Kimonge Kiravo akizungumza na Mhariri wa gazeti la Mwananchi Bw. Rashid Kejo.
Huu ni mmoja wa mitambo ya kuchakata mchanga wa madini mbalimbali ikiwemo Tanzanite katika mgodi huo.
Irene Mark Mhariri wa Gazeti la
Tanzania Daima akishiriki kazi ya kuchambua madini ya Tanzanite wakati
wahariri walipotembelea kiwandani hapo.
Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho akiendelea na kazi.
Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea na kazi katika mtambo wa kuchambua madini ya Tanzaniate.
Mkurugenzi mtendaji wa
Fullshangweblog Bw. John Bukuku pamoja na Mhandisi wa mgodi wa
Tanzanite One Bw. Anton Potigieter ambaye ni Meneja wa uchimbaji wa
madini chini ya Ardhini wakiwa wamevalia mavazi rasmi tayari kwa kushuka
mgodini mita 610 kwa ajili ya kujionea shughuli za uchimbaji
zinavyofanyika.
Mkurugenzi mtendaji wa
Fullshangweblog Bw. John Bukuku akiwa katika picha ya pamoja na
wahariri kutoka kulia ni Neville Meena Katibu wa TEF na Mhariri Mtendaji
wa Gazeti la Tanzania Daima, Jimmy Charles kutoka Gazeti la Rai na
kushoto ni Rashid Kejo Mhariri kutoka Gazeti la Mwananchi wakiwa
wamevalia mavazi rasmi tayari kwa kushuka mgodini Mita 610 ili kuona
shughuli za uchimbaji madini ya Tanzanite.
Hapa tukiwa tayari kwa kiungia mgodini
Tukiwa tayari kuingia mgodini katikati ni Mzee Theophil Makunga Mwenyekiti wa Jukwaa wa la Wahariri TEF.
Mmoja wa wachimbaji akiendelea na kazi chini ya Ardhi mita 610 katika mgodi wa Tazaniate One uliopo Kitalu C.
Baadhi ya wahariri wakiangalia
miamba ya madini ya Tanzanite katika mgodi wa Tanzanite wakati uchimbaji
ukiendelea mita 610 ardhini.
Mhariri wa Clouds Joyce Shebe akishuka kwenye kiberenge mara baada ya kuwasili na wenzake mgodini mita 610 chini ya ardhi.
Mkurugenzi wa Fullshangweblog Bw.
John Bukuku katikati akiwa katika picha ya pamoja na Jeniffer Sumi
mhariri wa Startv na Patricia Kimelemeta kutoka gazeti la Mtanzania
mgodini chini ya ardhi.
Baadhi ya wanahabari wakipata maelezo katika mgodi huo kutoka kwa mmoja wa wasimamizi wa uchimbaji madini.
Wachimbaji wakiendelea na kazi mgodini.
Wahariri wa vyombo mbalimbali
pamoja na baadhi ya wahandisi wa kampuni ya Tanzanite One walioongozana
nao wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kurejea juu kutoka
mgodini walipoutembelea mgodi huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni