Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi, Ajira,Vijjana
na watu wenye Ulemavu James Kajugusi (katikati) akipata ufafanuzi juu
ya kilimo cha mbogamboga toka kwa Mwenyekiti Kinondoni Saccoss Neema
Urio (Kulia) katika ufunguzi mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana
kulia mwa Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana ni Mkurugenzi Msaidizi Mafunzo
Idara ya Vijana Venerose Mtenga na kushoto ni Mkurugenzi Uhamasishaji
Idara ya Vijana Esther Riwa.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi, Ajira,Vijjana
na watu wenye Ulemavu James Kajugusi (katikati) akipata ufafanuzi juu
ya matumizi ya jiko linalotumia nishati ya jua toka kwa Meneja wa
Tanzania Agriculture Productivity Programme Praygod Mushi (Kulia) katika
ufunguzi mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kushoto ni Mkurugenzi
Uhamasishaji Idara ya Vijana Esther Riwa.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi, Ajira,Vijjana
na watu wenye Ulemavu James Kajugusi (mwenye koti la Draft) akitoa
ushauri kwa wajasiriamali toka Pop Up the Best Tailoring wa Sinza Dar es
Salaam walioshiriki mafunzo ya usajasiriamali yaliyofanyika Jijini Dar
es salaam, kushoto ni Mkurugenzi Uhamasishaji Idara ya Vijana Esther
Riwa.
Mkurugenzi
Uhamasishaji, Idara ya Vijana Esther Riwa akizungumza na washiriki
(Hawapo pichani) wa mafunzo ya ya kilimo cha kisasa kwa vijana
yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi Mafunzo Idara ya Vijana Venerose Mtenga akiongea na washiriki
wa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kushoto ni Mkurugenzi
Maendeleo ya Vijana taifa James Kajugusi.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi, Ajira,Vijjana
na watu wenye Ulemavu James Kajugusi akizungumza na washiriki (Hawapo
pichani) wa mafunzo ya ya kilimo cha kisasa kwa vijana yaliyofanyika
Jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya vijana wakimsikiliza mtoa mada(Hayupo pichani) juu ya juu ya kilimo
cha kisasa kwa vijna katika mafunzo yaliyofanyika Jiji Dar es salaam na
kushirikisha vijana toka Dar es salaam na pwani.
Mmoja
wa washiriki wa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana Bi. Jasmin John
akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya kufungua mafunzo
hayo yanayofanyika kwa siku tatu Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi, Ajira,Vijjana
na watu wenye Ulemavu James Kajugusi akipongezana na Mkurugenzi
Msaidizi Mafunzo Idara ya Vijana Venerose Mtenga mara baada ya
kufunguliwa kwa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijina yanayofanyika
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi, Ajira,Vijjana
na watu wenye Ulemavu James Kajugusi akisalimiana na Mwenyekiti wa
mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana Bi Mary Lucian Mdendemi mara
baada ya kufunguliwa kwa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijina
yanayofanyika jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi Uhamasishaji,
Idara ya Vijana Esther Riwa.Picha zote na Raymond Mushumbusi ( WHUSM)
Na Shamimu Nyaki-WHUSM 02/03/2016
Katika
kuboresha na kuongeza ajira hapa nchini Serikali imeahidi
kuwapatia Vijana mtaji na maeneo kwa ajili ya kilimo cha kisasa ili
waweze kujiendeleza na kukuza kipato chao.
Akizungumza
katika ufunguzi wa mafunzo ya kilimo cha kisasa cha “Green Houses”
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu,
Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu, Bw. James
Kajugusi amesema kuwa ni wakati muafaka kwa vijana kutumia fursa
mbalimbali zinazojitokeza katika kilimo kwa kuwa ndio uti wa mgongo wa
Taifa letu.
Ameongeza
kuwa Serikali inaendelea kuwawezesha kupata mikopo kwa riba nafuu na
kutoa elimu kuhusu kilimo bora cha kisasa ili kuondoa fikra zilizopo
kwa vijana kuwa kilimo ni kwa ajili ya watu waliokosa elimu,wenye maisha
duni na wale wanaoishi maeneo ya vijijini.
“Ni
lazima tutumie fursa zinazojitokeza katika kunufaika,nina imani
mtatumia fursa hii kwa manufaa yenu na elimu mtakayopata itawasaidia
kuzalisha bidhaa bora na kuondoa utegemezi. Alisema Mkurugenzi
Kajugusi”.
Aidha
mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw Praygod Mushi amewataka vijana hao
kuamini kuwa kilimo kinaweza kubadilisha maisha yao kama watatumia
fursa zote zinazojitokeza katika sekta ya kilimo kuanzia ngazi ya
familia mpaka Taifa.
Naye
mmoja wa washiriki katika mafunzo hayo Bi Jasmini John ameishukuru
Serikali kwa kuaandaa mafunzo hayo na kusema kuwa atatumia elimu
atakayopata kuendeleza kilimo kama ajira kwa kutumia pembejeo za kisasa
atakazoelekezwa katika mafunzo hayo.
Mafunzo
ambayo vijana hao wamepewa ni jinsi ya kutumia dawa na mbegu bora
katika kilimo,kunufaika na mazao yatokanayo na kilimo cha Green
House,utunzaji wa mazingira kwa kutumia Nishati ya mwanga wa jua pamoja
na ubunifu wa shughuli za vijana katika jitihada za kukuza viwanda kwa
kutumia mali ghafi za humu nchini.
Mafunzo hayo yanatolewa kwa siku tatu kuanzia leo na yameshirikisha vijana kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni