Golikipa mahili wa Mbeya City Fc, Juma K Juma amerejea kikosini
kutoa mapumziko ya majuma mawili aliyopewa na kocha Kinnah Phiri
kufuatia mkwewe Bi Nasra Nassor kujifungua watoto mapacha hivi
karibuni.
Akizungumza na mbeyacityfc.com muda mfupi uliopita Kaseja amesema
kuwa amefurahi kusafiri na hatimaye kurudi salama kwenye timu yake huku
pia akitoa shukurani zake za dhati wa wale wote ambao wamekuwa karibu
nae yeye kama mchezaji na pia familia yake tangu alipojiunga na City.
“Nashukuru mungu nimefika hapa salama baada ya safari
yangu, pia namshukuru kwa kile alichonijaalia, nimerudi kikosini nikiwa
na ari kubwa zaidi ili kuituikia timu yangu kwa nguvu zote katika
kutafuta mafanikio hasa kwenye kipindi hiki ambacho ligi inaelekea
mwishoni, hakika tunapita kwenye kipindi kigumu lakini umoja wetu
utatufanya kuvuka hapa” alisema.
Akiendelea zaidi Kaseja aliyewahi kucheza kwa mafanikio kwenye timu
za Moro United, Simba, na Yanga aliweka wazi kuwa anaimani kuwa na kocha
Kinnah Phiri kuwa ataijenga upya City na kuifanya kuwa timu
itakayotisha zaidi kwenye msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania
Bara.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni