SMILE YAONGOZA UFUMBUZI MPYA WA MATUMIZI YA HUDUMA YA 4G LTE

 Meneja Mkazi wa Kampuni ya Smile Tanzania Bw. Erick Bahner Akizungumza na Waandishi wa Habari ambao (Hawapo Pichani)


Katika harakati za kuhakikisha wateja wake nawatanzaniakwa Ujumla wanafikiwa na huduma mtandaoni zenye ubora wa hali ya juu, kampuni ya Smile Tanzania imetengeneza historia nyengine  nchini wa uzunduzi wa huduma mbili zinazotumia mtandao wa intaneti wa 4G LTE.

Akizungumzia juu ya uvumbuzi huo katika huduma za intaneti Meneja Mkazi wa kampuni ya Smile nchini, Bw. Eric Behner,ameeleza kuwa huduma hizoni SmileVoice inayowawezesha wateja kupiga simu mtandaoni ambayo ni ya kwanza nchini yenye kusikika kwa ubora mkubwa na SmileUnlimited ambayo inatoa fursa kwa mteja kutumia huduma ya intaneti bila kikomo ndani ya siku 30.

SmileVoice ni huduma ya hali ya juu inayopatikana kwenye vifaa vya Android na Apple iPhone kupitia app na kumwezesha wateja kupiga simu mtandaoni ikitumia huduma ya Smile 4G LTE na kumpa mteja uwezekano wa SuperClear voice yaani High definition.
“Smile ni kampuni ya kwanza ya huduma za mawasiliano ya simu duniani kuanzisha na kuendelezaprogramu ya bure ya huduma ya kupiga simu mtandao wa 4G LTE kutumia app. Huduma hiiinawawezesha wateja wetu nchiniTanzania wenye simu za Android na iPhone kufurahia kupiga simu zenye ubora wa hali ya juu kupitia intaneti yetu yenye kasi zaidi. Tumejizatiti kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha tunaboresha huduma za kupiga simu na mtandao wa intaneti. Kwa kupitia huduma ya Smile Voice, wateja wetu wanaweza kupiga simu nchinina nje ya nchi kama mitandao mingine ya simu.” Alisema Bw. Behner

“Mbali na huduma ya Smile Voice, Smile, kupitia kukusanya rasilimali za kutosha, Smile imefanikiwa kutanua huduma zake mtandao wa  4G LTE mpaka kufikia miji 7 nchini Tanzania  na sasa kuwapa fursa wateja kutumia intaneti bila kikomo ndani ya siku 30 yenye kasi zaidi. Hakuna kampuni nyingine nchiniinayotoa huduma kamahiyo zaidi ya Smile.” Aliongezea Bw. Behner
Akifafanua zaidi kuhusu huduma ya Smile Unlimited, Bw. Behner amesema kuwa huduma hiyo ipo ndani ya sera ya kampuni ya usawa katika matumizi. Sera hii itamfaidisha mteja kwani itamuhakikishia kuwa anakuwa ameunganishwa kwa uhakika ndani ya sikuzote 30.

Programu ya SmileVoice app inawawezesha wateja ambao hawanasimu za VOLTE uhakika wakupiga simu kupitia mfumo wa LTE wakiwawameunganishwa na mtandao wa intaneti wa Smile.

“Katika soko la Tanzania, watu wenye vifaa vinavyotumia Android ndivyo vinavyo ongoza na ukijumlisha na SmileVoice app, basi tunawahakikishia wateja wetu watakaosajili nasi watajionea na kujivunia  upigaji simu zenye ubora wa hali ya juu kupitia simu zao.” Aliongezea Bw. Behner

Ili kuweza kutumia huduma ya Smile Voice,inambidi mteja awe na SIM iliyosajiliwana akiwa na kifurushi cha Smile. Programu hii inaweza kupakuliwa (downloaded) kwenye simu zinazotumia mfumowa Android na za iPhone (IOS) na hufanyakazi mara tubaada ya mteja kujisajilinayo mara moja.
Wakati simu ikiwahaina intaneti ya mtandao wa Smile mteja anaweza kupiga simu kwenda simu nyingine ambayo imeunganishwa na mtandao wa intaneti wa 3G, Wi – Fi au nje ya nchi.

Kwa Masiliano zaidi;

Imetolewa na:
Linda Chiza
Smile Communications Tanzania
SmileVoice number: +255 662 222 221
Mobile: +255 758 811280
Email: linda.chiza@smilecoms.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni