Tukio la kutekwa ndege ya abiria ya Misri na
kupelekwa kisiwa cha Cyprus limemalizika huku abiria wote waliotekwa
wakiachiwa huru na mtekaji kujisalimisha.
Ndege hiyo ya shirika la EgyptAir Flight MS181
ilitekwa na abiria mmoja mwanaume ambaye alidaiwa kuvaa kiunoni
mkanda uliokuwa na milipuko.
Maafisa wa shirika la ndege la Misri wamesema
wameambiwa na mamlaka za Cyprus kuwa mkanda huo wa mabomu ulikuwa ni
feki.
Abiria wakishuka kwenye ndege ya Misri iliyotekwa
Abiria walioshuka wakiwa kwenye uwanja wa ndege wa nchini Cyprus baada ya kuachiwa huru na mtekaji
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni