WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekagua hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera na
kumpa siku tano Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Adam Swai amletee
taarifa juu matumizi ya sh. Milioni 80 ambazo ni fedha za UKIMWI.
Pia
amemtaka ifikapo Machi 20, nwaka huu awasilishe taarifa nyingine ya
matumizi ya sh. Milioni 40 za ukarabati wa jengo la wagonjwa maalum
(Grade A)
Ametoa
agizo hilo leo asubuhi (Jumanne, Machi 15, 2016) wakati akizungumza na
watumishi wa hospitali hiyo baada ya kutembelea maeneo kadhaa yakiwemo
wodi ya watoto, wodi ya wazazi, chumba cha wagonjwa mahututi (ICU ) na
chumba cha kuhifadhia maiti.
"Kulikuwa
na frsha za ukimwi sh. Milioni 80 ambapo kila mtumishi alipaswa kupata
sh. 200,000/- lakini ninyi mmewapa sh. 80,000 /-. RAS fedha hizi
zimeenda wapi? Nataka uniletee taarifa ofisini kwangu Dar es Salaam
ifikapo tarehe 20 mwezi huu," alisema huku akishangiliwa.
"Kwa
mujibu wa taarifa ya CAG pale grade A kuna mgogoro wa sh. milioni 40.
Wewe taarifa unayo lakini hujaifanyia kazi yoyote. Nataka tarehe 20
nayo hii pia niipate na nione umetoa mapendekezo gani."
Kuhusu
tatizo la madaktari katika hospitali hiyo, Waziri Mkuu alisema
atawasiliana na Waziri wa Afya ili madaktari watano ambao wanasubiri
ajira rasmi lakini wameanza kazi kwa mkataba hospitali hapo wapewe ajira
rasmi. Pia alisema amebaini upungufu wa madaktari bingwa uliopo katika
hospitali hiyo.
Pia
aliahidi kufuatilia maombi yao ya gari la wagonjwa hasa ikizingatiwa
kuwa anayo maombi kama hayo kutoka hospitali za Mawenzi (Kilimanjaro),
na Ligula (Mtwara).
Katika hatua nyingine,
Waziri Mkuu aliwapongeza watumishi wa hospitali hiyo kwa huduma zao
nzuri wanazotoa kwa wagonjwa. "Nineridhishwa na kauli walizotoa
wagonjwa juu yenu. Tofauti na hospitali nyingine nilizopita, wao
wamesema hawajatozwa fedha ili wapatiwe dawa. Nimefarijika sana."
"Endeleeni
kuwa na huruma kwa wagonjwa. Endeleeni kuwa na lugha nzuri kwa
wagonjwa. Hawa wagonjwa hawakuogopa kuelezea hisia zao. Wamesema kwa
uwazi kabisa kwamba mnawajali," alisema.
Mapema,
akisoma taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk.
Thomas Rutachunzibwa alisema hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu
mkubwa wa madaktari bingwa pamoja na madaktari wa kawaida.
"Tunao
madaktari 10 lakini wanaohitajika ni 30. Tunao madaktari wasaidizi
wanane lakini wanaohitajika ni 23 na madaktari bingwa waliopo ni watatu
tu lakini wanaohitajika ni 24. Tunaomba tupatiwe watumishi hawa ili
tuweze kutoa huduma kulingana na matarajio ya wananchi wetu," alisema.
Akifafanua
kuhusu mahitaji ya hospitali hiyo, Dk. Rutachunzibwa alisema wanahitaji
sh. bilioni 1.8 kwa mwaka bila ya kuweka mishahara ili waweze kufanya
kazi yao kwa umakini. "Tunahitaji sh. milioni 802 kwa ajili ya matumizi
ya kawaida lakini tunachopokea hivi sasa ni sh. milioni 299 ambayo ni
sawa na asilimia 30 ya mahitaji yetu."
"Bajeti
ya dawa tuliyotenga ni sh. milioni 960 lakini tunapokea sh. milioni 143
ambazo kiuhalisia zinatosha kwa matumizi ya miezi miwili tu.
Tumelazimika kufanya marekebisho ya bei za dawa kwa ridhaa ya Bodi ya
hospitali ili tuweze kumudu kutoa huduma kwa wananchi," alisema.
Alisema
ili kubana mianya ya upotevu wa mapato, wanahitaji kuwa na kompyuta 15
lakini hadi sasa wamefanikiwa kununua kompyuta mbili tu ambazo ziko
Grade A na idara ya wagonjwa wa nje (OPD) ili kuimarisha utaratibu wa
ukusanyaji mapato.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, MACHI 15, 2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni