Serikali
 imewapongeza wadau kwa kutoa huduma za chanjo ya ugonjwa wa Kisukari 
ikiwemo kusaidia vijana wadogo wanaosomea masomo mbalimbali ya kisayansi
 hapa nchini.
Akizungumza
 wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la tatu la ugonjwa wa Kisukari 
kwa nchi za Afrika Mashariki,Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya na 
Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi 
Kigwangalla, amebainisha kuwa Serikali kupitia wizara hiyo ina mpango 
kabambe wa kuhakikisha inapambana na tatizo la ugonjwa wa Kisukari hapa 
nchini ambapo pia amewataka wadau wasichoke kushirikiana katika 
mapambano hayo.
Aidha,
 amewapongeza vijana walio katika vyuo vikuu hapa nchini licha ya kupata
 tiba ya ugonjwa wa Kisukari, lakini kwa hali yao hiyo bado wana moyo wa
 kusoma kuhakikisha wanafika mbali hivyo Serikali inajisikia faraja na 
kuwataka wadau kuwa na moyo huo huo wa kusaidiana na Serikali.
Kwa
 upande wao baadhi ya washiriki wakiwemo vijana wanafunzi na wengine 
wakiwemo waliotoa igizo namna ya ugonjwa Kisukari jamii unavyouweka 
kando, wameeleza kuwa kitendo cha dozi ya Kisukari kuuzwa kinawapa shida
 watu wengi kwani wapo wanaopoteza maisha kwa kukosa pesa za kutumikia 
dozi hiyo.
Hata
 hivyo, walimuomba Naibu Waziri Dk. Kigwangalla kuhakikisha Serikali 
wanaliangalia hilo ili dozi ya Kisukari yaani Insulini, ipatikane bure 
kwa watumiaji wake.
Kongamano
 hilo lililozinduliwa jana Machi 14.2016, ni la siku tatu na 
linatarajiwa kufikia tamati, kesho Machi 16.2016. Ambapo linajumlisha 
wataalaam wa utafiti wanasayansi katika ugonjwa wa Kisukari ( pre – 
congress training – applied research in diebetes) na kuandaliwa na asasi
 inayojulikana kama (EADSG) The Eafrica diabetes study group. 
Asas hii ilianzishwa mwaka 2011 ili kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa huo na kuutafiti pamoja na kutafuta tiba.
Awali
 akiongea na waandishi wa Habari, Mratibu wa Kongamano hilo Doctor 
Kaushik Ramalya, amesema wageni mbalimbali wapo katika majadiliano na 
uchunguzi huo wa Kisayansi, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu wa 
namana ya kutua matatizo yatokanayo na ugonjwa huo.
UTAFITI:
Aidha
 utafiti uliotolewa hivi karibuni umeonyesha kuwa katika kila sekunde 
sita mtu mmoja hufa kutokana na ugonjwa wa kisukari ( vifo zaidi ya 
milioni 5.0 hutokea duniani). Mmoja katika watu wazima 11 ana ugonjwa wa
 kisukari ( watu milioni 415 duniani kote wanaishi na Kisukari). 
Moja
 katika vizazi saba, huadhirika na ugonjwa wa kisukari katika kipindi 
cha ujauzito na kujifungua.Robo tatu (75%) ya watu wenye ugonjwa wa 
kisukari wanaishi katika nchi chini na kipato cha kati. 
Zaidi
 ya watu wazima wengi wanakufa kutokana na ugonjwa wa kisukari kuliko 
kutokana na VVU / UKIMWI, kifua kikuu na hata malaria.wastani wa milioni
 14.2 watu wazima wenye umri kati ya 20-79 wana ugonjwa wa kisukari 
katika Kanda ya Afrika. 
Afrika
 inaongoza kwa wagonjwa wa kisukari ambao haujatambuliwa, kutokana na 
kutocheki afya zao; zaidi ya 66.7 % ya watu wenye ugonjwa wa kisukari 
hawajui kuwa wana ugonjwa wa kisukari. 
Mtu
 ana kisukari aina ya 2 (Type 2 Diabetes) anaweza kuishi kwa miaka 
kadhaa bila kuonyesha dalili yoyote, madhara yanayoweza kujitokeza ni 
pamoja na ugonjwa wa figo , moyo kushindwa kufanya kazi, ugonjwa wa 
jicho na kusababisha upofu na matatizo ya mguu na kusababisha ulema.
Mataifa
 ya Afrika kwa idadi kubwa ya watu wenye ugonjwa wa kisukari ni pamoja 
na Afrika Kusini (2.3 milioni ), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (1.8 
milioni ) , Nigeria ( milioni 1.6 ) na Ethiopia (1.3 milioni).
Mgeni rasmi, Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla akisalimiana na wageni wengine waalikwa katika mkutano huo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni