…………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu,Johhanesburg
Jumla ya waogelaji nane wa timu 
ya Tanzania Swim Squad (TSS) watakuwa na ratiba ngumu kesho ya kuwania 
medali mbalimbali katika siku ya pili ya mashindano ya Kimataifa ya 
Afrika Kusini “South Africa Level 2” yaliyoanza jana kwenye bwawa la 
kuogelea la Ellis Park.
Waogeleaji hao ni Celina 
Itatiro, Marin de Villard,  Adil Bharmal, Amani Dogart, Josephine 
Oosterhuis, Jacquelene Kortland,  Isabella Kortland, Pieter De Raadt, 
Celina Itatiro na Marin de Villard.
Waogeleaji hao  watawania medali
 katika mashindano ya mita 50, 100, 200 na relay katika kwa upande wa 
wanawake na wanaume  kwa kushindana na waogeeaji wengine kutoka nchi za 
Zimbabwe, Msumbiji, Namibia na wenyeji Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa ratiba 
iliyotolewa  na waandaaji, Adil ndiye ataanza kuwania medali kwa uande 
wa Tanzania kwa waogeaji wenye umri  miaka 16  na kufuatiwa na Marin kwa
 upande wa mita 200 freestyle kwa waogeleaji wa wa miaka 11 na baadaye 
wasichana, Celina na Amani kushindana kwa upande wa wanawake wenye umri 
wa miaka 11 katika staili ya free style.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Adil
 na Marin wataingia tena kwenye ‘maji’ kushindana katika staili ya 
breaststroke mita 100 kwa upande wa umri wao ns baadaye Josephine na 
Jacqueline watapambana kwa watoto wenye umri wa miaka 15 na kufuatiwa na
 Celina na Amani tena.
Baada ya kushindana katika 
staili hizo mbili (freestyle na breaststroke mita 100 na 200), 
waogealeaji, Adil na Marin wataingia tena mashindananoni kuwania medali 
kwa upende wa mita 50 backstroke na baadaye Isabela Kortland, Josephine,
 Amani na Celina watawania medali tena.
“Ni ratiba ngumu sana kwa 
waoageaji wetu, ila tunashukuru kuwa wameweza kufanya mazoezi na kidogo 
kuzoea hali ya hewa ya ubaridi, sisi (TSS) tutatokea mji wa joto inaweza
 kutupa shida kwani baridi ya huku inaambatana na jua la kuchoma, si hai
 nzuri, ila tutajitahidi,” alisema Alex Mwaipasi.
Mwaipasi ambaye yupo na kocha 
mwenzake, Michael Livingstone alisema kuwa mashindai hayo ni magumu sana
 kutokana na idadi ya waogeleaji na idadi ya mashindano ambayo kila 
muogeleaji atashindana.
“Celina anatarajia kushindana 
katika mashindano tofauti 11, si mchezo na waogeleaji wpo zaidi ya 1000,
 nchi nyingi za ukanda wa Kusini mwa Afrika wameleta waogeaji, ni 
mashindano mazuri kwa kuwapa uzoefu waogeleaji wetu,” alisema Michael.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni