Mchezaji tenesi namba moja na bingwa
mtetezi, Serena Williams ameondolewa katika raundi ya nne ya michuano
ya Wazi ya Miami.
Katika mchezo huo Mmarekani Serena
alipoteza mchezo kwa seti 6-7 (3-7) 6-1 6-2 dhidi ya Mrusi Svetlana
Kuznetsova, na kuondolewa mapema mno katika michuano hiyo.
Serena Williams, 34, aliyetwaa
mataji 21 ya Grand Slam alikuwa akijaribu kushinda taji lake la tisa
la michuano hiyo ya wazi ya Miami.
Serena Williams akishindwa kujizuia kuonyesha huzuni kwa kuondolewa
Svetlana
Kuznetsova akizuia mpira uliopigwa na Serena Williams katika mchezo huo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni