Maafisa
wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa Kusini Pemba, wakisubiri usafiri wa
kuvukia kwelekea kisiwa Panza, kusikiliza matatizo ya wananchi
yaliyopelekea kutokuvuushwa kwa baadhi ya wananchi wanaishi kisiwa
hicho.
Viongozi mbali mbali wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa kusini
Pemba, wa kiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mkuu wa Mkoa wa kusini
Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla wakiwasili katika kisiwa Panza kwa
boti ya Kikosi cha KMKM.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma
Majid Abdalla akiwa katika harakati za kutaka kushuka katika faiba ya KM
KM baada ya kuwasili katika kisiwa Panza kutoka Chokocho, kwa lengo la
kuja kutatua mzozo uliopelekea baadhi ya wananchi kutokuvuushwa kwa
madai ya kisiasa
Wananchi
wa Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama Mkao kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdall, wakati
alipokuwa akizungumza nao kufuatia baadhi ya wananchi kukataliwa
kuvushwa kisiwani huko kwa madai ya itikadi za kisiasa
Mwenyekiti
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa kusini Pemba Mhe: Mwanajuma
Majid Abdalla akiwa na viongozi mbali mbali wa serikali katika kisiwa
Pemba, kwa lengo la kukagua mazingira ya kisiwa hicho.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalla, akitoa maelezo kwa
wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa kusini Pemba, wakati
walipowasili katika kisiwa Panza kusikiliza matatizo yaliyopelekea
baadhi ya wananchi kutokuvuushwa kwa madai ya kisiasa.(Picha na Abdi
Suleiman, PEMBA.)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni