MGODI WA BULYANHULU WAALIKA WANAWAKE KUJIONEA UCHIMBAJI MADINI YA DHAHABU CHINI YA ARDHI

Mfanyakazi wa mgodi wa kuchimba dhahabu wa Bulyanhulu, unaomilikiwa na kampuni ya Acacia, akiwa na baadhi ya akina mama sehemu ya uchimbaji chini ya ardhi (underground mining), wakati akina mama wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo na wafanyakazi wa kike walipotembelea ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake Duniani, leo Machi 8, 2016. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said, Bulyanhulu
KATIKA kuadhimisha kilele  cha siku ya Wanawake Duniani leo Machi 8, 2016, akina mama wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, unaomilikiwa na kampuni ya Acacia,huko wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, wao walitembelea na kuona shughuli za uchimbaji madini chini ya ardhi (Underground operations).
Akina mama hao kutka kada mbalimbali za vikundi vya wajasiriamali, wakulima, na viongozi wa dini, walifanya ziara ya kutembeela na kujionea shughuli za uchimbaji madini chini ya ardhi kiasi cha kilomita 2 kutoka uso wa ardhi, walieleza kufurahishwa kwao na kusema hata wao wanaweza.
Pamoja na maeneo waliyoyatembelea, walijionea mashine za kuchironga miamba, pamoja na karakana (gereji) ya kutengeneza magar na mashine zinazotumika kwenye eneo hilo. Ziara hiyo iliwachukua takriban masaa matatu (3), na bila kuchoka walikamilisha  ziara hiyo na wote walikuwa katika hali nzur nay a furaha.
Katika tukio linguine, Mgodi huo ulimpatia kila mshiriki wa ziara hiyo, mche moja wa matunda ili wakapande kwenye maeneo wanayoishi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya mgodi kuhifadhi mazingira kwenye maeneo jirani na mgodi huo.
Siku ya wanawake Duniani, huadimishwa Machi 8 ya kila mwaka ili kuelezea changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake na kutafuta majawabu yake.



 Mama huyu ambaye ni sister wa kanisa Katoliki, alikuwa miongoni mwa wanawake waliotembelea mgodi huo chini ya ardhi


 Ramadhani Chura, (kulia), mchimbaji wa madini chini ya ardhi, akiwapa maelezo akina mama hao umbali wa kilomita 2 kutoka uso wa ardhi
 Mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu akimsaidia mama huyu akuvaa kibuyu cha gesi ya oxygen kabla ya kushuka chini ya ardhi
 Mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu akimuwekea kibuyu cha gesi ya Oxygen mama huyu tayari kaunza safari chini ya ardhi
 Mkuu wa Uhusiano na mawasiliano wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, Mary Lupamba, (kulia), akimsaidia mama huyu kuweka sawa kibuyu chake cha gsi ya Oxygen ili kutembelea eneo la uchimbaji chini ya ardhi
 Hapa akina mama wako chini ya ardhi umbali wa kilomita 2 kutoka uso wa ardhi, wakipatiwa maelezo ya namna miamba inavyochorongwa kuipata dhahabu
 "Wanawake tunaweza". ndivyo inavyoonekana kwa mama huyu akidandia gari la oeperesheni za chini ya ardhi kwenye mgodi wa Bulyanhulu wakati akina mama wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo walipoadhimisha siku ya wanawake kwa kutembelea na kujionea kazi ya uchimbaji madini chini ya ardhi
 Mwendesha mashine kubwa akiwa kwenye mashine yake
 Mtaalamu wa kuchoronga miamba chini ya ardhi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, akiwapatia maelezo ya namna kazi hiyo inavyofanyika
 Akina mama hao (kulia), wakiingia kwenye lango la kuelekea kupanda lifti ya kuwashusha chini ya ardhi
 Hawa ndio akina mama shujaa waliomudu kutembelea mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu chini ya ardhi kujionea kazi ya uchimbaji madini inavyofanywa, wakiwa na baadhi ya wafanyakazi wanaohudumu kwenye eneo hilo
 Mary akiwaongoza akina maam hao katika hatuaya awali ya kuelekea kwenye ziara ya chini ya ardhi
 Fundi mitambo akiwa kwenye karakana (gereji) ya magari na mashine zinazofanya kazi kwenye eneo hilo
 Akina mama shujaa wakiwa katika picha ya pamoja
Baadhi ya akina mama wakiwa chini ya ardhi umbali wa kilomita 2 kuona kazi ya uchimbaji madini inavyofanywa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni