Naibu
 Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na 
Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (katikati) akiwasili kwenye uzinduzi wa 
ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 
2015) huku akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa 
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez 
(kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa 
Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kulia) uliofanyika Machi 11,
 2016 jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Naibu
 Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na 
Walemavu) Antony Mavunde ametaka kuondolewa kwa changamoto maeneo ya 
kazi ili kazi isaidie maendeleo ya binadamu badala ya kujikimu.
Naibu
 Waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari
 baada ya kuzindua ripoti ya  maendeleo ya binadamu ya mwaka 2015 
inayoelezea kazi kwa maendeleo ya binadamu.
Alisema
  kwa sasa kuna figisu kubwa katika kazi nchini hasa kutokana na  
waajiri wengi kugeuza kazi kama sehemu ya kujikimu kwa wafanyakazi wao 
kwa kutowapa stahiki husika ikiwamo mikataba ya ajira.
Alisema
 kazi inapokuwa ni ya kujikimu kunakuwa na migogoro mingi na kuvurugika 
kwa uzalishaji na kutishia maendeleo ya taasisi husika na maendeleo ya 
mtu binafsi.
Alisema
 Tanzania imefurahishwa na yaliyomo katika ripoti hiyo ya Shirika la 
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kutokana na kuzungumzia jinsi kazi 
zinavyoweza kusaidia upatikanaji wa maendeleo.
Alisema
 wakati Tanzania inaelekea kujipanga kwa uchumi wa kati, Ripoti 
inaonyesha ni jinsi gani kazi inaweza kuboresha maisha ya Mtanzanzania 
kwa kuondoa kazi na kuwapatia wananchi kazi zenye staha na zinazoweza 
kuwasaidia wao binafsi na hivyo kukuza uchumi na ustawi wa jamii.
Alisema
 amekuwa akizungumza katika maeneo mengi ya kazi na kukutana na 
changamoto nyingi zikiwemo za kukosekana kwa mikataba, mazingira mabaya 
ya kufanyakazi, ujira usiokidhi na kutaka waajiri kufuata sheria za kazi
 kwa kuwapatia mikataba ya kazi na pia kuhakikisha kazi zinakuwa na 
staha.
Awali
 akizungumza na wageni waalikwa katika hafla hiyo iliyofanyika mwishoni 
mwa wiki  mjini Dar es Salaam, alisema kwamba uzinduzi wa kitaifa ambao 
unafuatia uzinduzi wa kimataifa uliofanyika mwaka jana mjini Addis 
Ababa, Ethiopia  ni faraja kubwa kwa wadau wa maendeleo nchini.
Alisema
 uzinduzi huo unaweka ripoti hiyo karibu zaidi na wananchi na kuahidi 
serikali kuifanyia kazi kutokana na umuhimu wake hasa wa kuhakikisha 
kazi inasaidia maendeleo ya watu.
Naibu
 Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na 
Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (kushoto) akibadilishana mawazo na 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika 
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (katikati) pamoja na Mkurugenzi 
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi 
Kida (kulia) kabla ya kuelekea kwenye uzinduzi rasmi wa ripoti ya 
maendeleo ya watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) 
uliofanyika Machi 11, 2016 jijini Dar es Salaam na kuratibiwa na ESRF.
Anasema ripoti hiyo inaonesha namna ambavyo kazi inaweza kuchangia maendeleo na ustawi wa jamii.
Alisema
 wakati Tanzania inaelekea kuwa taifa ambalo limejengeka katika msingi 
wa maendeleo ya watu  kama ilivyokusudiwa tangu kupatikana kwa Uhuru 
wake 1961, Ripoti hiyo ni chanzo kizuri cha maarifa katika kufanikisha 
mabadiliko yanayotakiwa kufanikisha maendeleo ya watu.
Alisema
 kazi ni msingi wa maendeleo kwa hiyo ni vyema kuboresha mazingira ya 
kazi na wafanyakazi ili kuleta maendeleo kusudiwa kwa kuwa na kazi zenye
 staha.
Alipongeza
 UNDP na wadau wengine kwa kufanikisha uzinduzi huo ambao alisema 
umeenda sanjari na dhima ya serikali ya kutumia maarifa yote yaliyopo 
kusaidia maendeleo ya watu.
Ripoti hiyo ya UNDP imetazama kwa undani kuhusu kazi, mahusiano ya kazi na maendeleo ya binadamu.
Mshehereshaji
 wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human 
Development Report 2015) akisherehesha uzinduzi huo uliofanyika Machi 
11, 2016 jijini Dar es Salaam na kuratibiwa na ESRF.
Aidha
 imeangalia masuala ya usalama wa kazi na mahitaji ya utaalamu; masuala 
ya kulipwa na kutolipwa kazini, uangalizi, kujitolea ubunifu na kazi 
endelevu.
Pia
 ripoti hiyo inatoa majumuisha yanayostahili kufanywa bali mapendekezo 
ya utengenezaji wa sera unaotanua uzalishaji kwa kutoa fursa na kulinda 
wafanyakazi, ubora wa kazi, ujira stahiki, kazi yenye staha na kazi 
endelevu  kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Kimsingi
 Ripoti hiyo inapendekeza kuongeza faida za maendeleo ya binadamu,  
kupitia utendaji kazi, kwa kupendekeza mikakati ya kujenga fursa za 
ajira, ili kuhakikisha ustawi wa wafanyakazi, na kuendeleza maeneo 
yaliyolengwa, ambayo yatabadilisha hali halisi ya sasa.
Aidha
 ainaangalia Sera zilizopendekezwa, kuhakikisha utendaji kazi bora, 
utendaji kazi endelevu, ambayo inachangia usawa, badala ya kujenga 
ukosefu wa usawa, na kazi ambayo inaheshimu haki za wafanyakazi, na 
kuhakikisha usalama wao.
Mratibu
 Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisoma taarifa kwenye uzinduzi wa 
Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 
2015) uliofanyika jijini Dar es Salaam Machi 11, 2016 na kuratibiwa na 
ESRF.
Kwa
 mujibu wa ripoti hiyo kuna hatua njema kwenye maendeleo ya watu katika 
ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania ikiwamo lakini ipo haja 
ya kuangalia  pengo kubwa lililopo katika fursa mbalilmbali zikiwamo za 
kazi.
Imeelezwa
 ndani ya ripoti hiyo kwamba toka mwaka 2000 nchi ziloizo kusini mwa 
Jangwa la Sahara zimekuwa na ukuaji wa maendeleo ya binadamu( Human 
Development Index -HDI)  wa kazi wa kiwango cha asilimia 1.7 kati ya 
mwaka 2000 na 2010 : asilimia 0.9 kwa mwaka  2010 na 2014.
HDI ni kipimo kinachotathmini maendeleo ya muda mrefu  ya afya na maisha marefu, elimu na maisha yenye staha.
Kwa
 Tanzania  kumekuwepo na  ongezeko la HDI la asilimia  1.18% kati ya 
mwaka 1985 na 2014, ikiongezeka kutoka 0.371 hadi  0.521,  ikiwa ni 
ongezeko la asilimia 40.5  juu ya ongezeko la nchi zilizo kusini mwa 
Jangwa la Sahara la 0.518.
Mkurugenzi
 Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
 Kida akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu 
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na 
Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (hayupo pichani) kuhutubia wageni 
waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya 
mwaka 2015 (Human Development Report 2015) uliofanyika jijini Dar es 
Salaam Machi 11, 2016 na kuratibiwa na ESRF.
Mratibu
 wa Umoja wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Mwakilishi
 wa Shirika la Maendeleo (UNDP),  Alvaro Rodriguez akizungumza katika 
uzinduzi huo alisema kwamba ongezeko hilo si haba.
Hata
 hivyo aliwaambia wadau waliokuwepo kushuhudia uzinduzi huo kwamba Taifa
 bado linakabiliwa na changamoto nyingi zikkiwemo umaskini uliokithiri, 
kutanuka kwa pengo la usawa na kushindwa kuhimili matukio ya mabadiliko 
ya tabianchi na uchumi.
Aidha
 alisema kwamba :”Ripoti ya maendeleo ya binadamu ya mwaka 2015, 
inaonyesha kuwa, kuimarisha maendeleo ya binadamu, kupitia utendaji 
kazi,  inahitaji sera na mikakati katika maeneo makuu matatu: kujenga 
fursa za ajira, kuhakikisha ustawi wa wafanyakazi na kuendeleza maeneo 
yaliyolengwa. Hii inaongeza kasi ya kutengeneza ajira nchini Tanzania.”
Tanzania
 ikiwa na zaidi ya watu milioni 12 wakiishi katika umaskini na wengi wao
 uliokithiri changamoto kubwa  kwa Tanzania, ni kutafsiri uwezo huu 
katika miundombinu inayoonekana, kwa kujenga mazingira mazuri,  na 
kuongeza ujuzi wa watu wake kama ilivoainishwa katika Ripoti ya 
Maendeleo ya Binadamu mwaka elfu mbili na kumi na tano.
Naibu
 Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na 
Walemavu), Mh. Anthony Mavunde akisoma hotuba ya uzinduzi wa Ripoti ya 
Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) kwa 
niaba ya Waziri Jenista Mhagama, uliofanyika jijini Dar es Salaam Machi 
11, 2016 na kuratibiwa na ESRF.
Alisema
 changamoto zote hizo ni za kweli na zenye uhusiano na maendeleo ya 
binadamu na ni vyema ilivyowekwa katika Muono wa maendeleo ya Tanzania 
kufikia 2025 na utekelezaji wa malengo  ya maendeleo endelevu (SDGs).
Katika
 hotuba yake ya shukurani Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo, 
alisema kwamba  taasisi yake ipo tayari kusaidia Tanzania na nchi 
nyingine kuwezesha kutambua uhusiano kati ya  kazi na maendeleo ya 
binadamu katika utekelezaji wa Maendeleo endelevu (SDGs).
Mgeni
 rasmi  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, 
Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (katikati) na meza kuu 
wakijiandaa kuzindua ripoti hiyo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa 
Shirika la Kazi  Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, 
Bi. Mary Kawar, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na 
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkurugenzi 
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi 
Kida pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la 
Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo.
Mgeni
 rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, 
Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (katikati) akizindua rasmi 
Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 
2015) kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Machi 11, 2016.
Mgeni
 rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, 
Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde akionyesha ripoti hiyo kwa 
wageni waalikwa na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Kutoka
 kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Kazi  Ofisi ya Tanzania, Kenya, 
Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
 Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro 
Rodriguez, Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, 
Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde, Mkurugenzi 
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi 
Kida pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la 
Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo kwa pamoja wakiwa wameshikilia ripoti 
hiyo.
Muonekano wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015). 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni