Wananchi wa Pakistani wanaomboleza
vifo vya watu 70, vikiwemo vya watoto 29 vilivyotokea katika
shambulizi la Jijini Lahore.
Serikali ya Mkoa wa Lahore
imetangaza siku tatu za maombolezo, na siku moja ya maambolezo
imetangazwa katika maeneo mengine Pakistani.
Kundi lililojitenga kutoka kwa
Taliban la Jamaat-ul-Ahrar limekiri kufanya shambulizi hilo
lililowalenga Wakristo waliokuwa wakisherehekea Sikukuu ya Pasaka,
ambapo watu 300 walijeruhiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni