Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba akielezea
matumizi ya intaneti yalivyo nchini na changamoto zinazowakabili
watumiaji wa huduma hiyo.
Mwaka
2016 unakuwa mwaka wa neema kwa Tanzania kupata fursa ya kuandaa Mkutano
unaowakutanisha wadau wa intaneti (African Peering and Interconnection
Forum), mkutano unaotaraji kufanyika Agosti 31 – Septemba 1, jijini Dar
es Salaam.
Akizungumzia
mkutano huo, Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet
Society, Michuki Mwangi amesema mkutano huo unalengo wa kukutanisha
wadau mbalimbali wa intaneti ili kutanua miondombinu ya intaneti katika
bara la Afrika.
Amesema
taasisi yake inapenda kuona huduma ya intaneti ikipatikana kwa urahisi
kwa watumiaji wake Afrika na hivyo kupitia mkutano huo wataweza kutazama
jinsi gani wanaweza kushirikiana na kubadilishana takwimu za watumiaji
wa mitandao kwa bara zima la Afrika.
“Tunatambua
kuwa watumiaji wa intaneti wanazidi kuongezeka na kupitia mkutano huu
tutaweza kuangalia jinsi gani tunaboresha huduma ya intaneti iwe bora
ili iweze kutumiwa na watu wengi zaidi,” amesema Mwangi.
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba
amesema mkutano huo una umuhimu kwa Watanzania kwa kupata fursa ya
kujifunza na kubadilishana mawazo na watu kutoka mataifa mengine katika
huduma ya intaneti.
Amesema
kwa sasa Tanzania bado ina changamoto nyingi katika huduma ya intaneti
na kupata nafasi hiyo ya kuandaa mkutano kutakuwa na faida kwa mashirika
yanayotoa huduma ya intaneti ili kuwawezesha kutambua ni jinsi gani
wataboresha huduma kwa wateja.
“Nchi
yetu inawatumiaji wengi wa intaneti ila bado kuna changamoto nyingi
ikiwepo usalama wa mtandao na serikali inafanya jitihada nyingi kumaliza
changamoto hizo na kupitia mkutano huu tunaamini utasaidia zaidi
Watanzania kupata kitu kipya katika huduma ya intaneti,” amesema Simba.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary amesema Watanzania wengi
bado hawajafahamu umuhimu wa intaneti kutokana na kutokuwa na ujuzi wa
kutosha kuhusu intaneti lakini kupitia mkutano huo ulioandaliwa na
Internet Society wataweza kuapata elimu mpya kuhusu intaneti.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba (kushoto)
akizungumza jambo na Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary.
Wa
kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini
(TCRA), Dkt. Ally Simba (kushoto), Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary,
Meneja Mradi wa Tanzania Internet Exchange (TIX), Frank Habicht na
Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki
Mwangi wakizungumza jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary akifungua mkutano huo.
Meneja
Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi
akizungumzia mkutano wa Intaneti, AfPIF utakaofanyika nchini, Agosti, 30
- Septemba, 1
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo.
Baadhi ya waandishi waliohudhuria mkutano huo.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni