LIVERPOOL YATAKATA NA KUICHAPA MAN UTD 2-0 LIGI YA EUROPA

Liverpool imeendelea kutakata katika Ligi ya Europa baada ya kuanza kuiweka kando ya michuano hiyo Manchester United yenye kiwango kibovu katika mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa katika dimba la Anfield.

Kikosi cha Jurgen Klopp kilitawala mchezo huo wa kwanza wa baina ya timu hizo mbili kuu za Ligi Kuu ya Uingereza, na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Daniel Sturridge na Roberto Firmino kufunga la pili.

Katika mchezo huo Manchester United haikutengeneza nafasi yoyote ya maana ila iliendelea kubebwa na kipa wao David de Gea aliyezuia michomo ambayo ingeipatia Liverpool magoli zaidi ya hao mawili.
          Clyne akichuana na Memphis Depay wa Manchester United kuwania mpira
              Kocha wa Liverpool Jurgen Kopp akishangilia moja ya bao lililofungwa

Matokeo mengine ya Ligi ya Uropa ni Bor Dortmd 3-0 Tottenham, Ath Bilbao 1-0Valencia, Basel 0-0 Sevilla, Fenerbahçe 1-0 Sporting Braga, Shakt Donsk 3-1 Anderlecht, Sparta Prague 1-1 Lazio na Villarreal 2-0 Bayer Levkn.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni